Pata taarifa kuu

Sudan: Umoja wa Mataifa wasikitishwa na kuongezeka kwa mapigano El Fasher

Kwa zaidi ya mwaka mmoja, na kuanza kwa vita kati ya jeshi la serikali la Jenerali Abdel Fattah al-Burhane na Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Jenerali Hemmedti, El Fasher, jiji kubwa zaidi la Darfur, linasalia mikononi mwa jeshi la serikali. Lakini wanajeshi wa Jenerali Hemmedti wamekuwa wakiuzingira mji huo kwa wiki kadhaa na mapigano makali yameripotiwa. Umoja wa Mataifa una wasiwasi zaidi kuliko hapo awali.

(kumbukumbu) Uharibifu baada ya milipuko ya mabomu huko El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, Septemba 1, 2023.
(kumbukumbu) Uharibifu baada ya milipuko ya mabomu huko El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, Septemba 1, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Hofu inazidi kukutanda nchini Sudan, huko Darfur magharibi mwa nchi. Mikoa ya Darfur kwa kiasi kikubwa inadhibitiwa na wanamgambo wa FSR wa Jenerali Hemmedti. Ikiwa jiji kubwa zaidi la Darfur, El Fasher, likisalia mikononi mwa jeshi la Jenerali Burhan na washirika wake, kwa wiki kadhaa RSF imekuwa ikiuzingira mji huo, mji mkuu wa jimbo la Kaskazini la Darfur. Kuna mapigano. RSF imeharibu vijiji, na jeshi lilijibu kwa mabomu maeneo ambayo raia wanaishi.

Matumizi ya silaha nzito

Wito wa kumaliza mzingiro umeongezeka katika wiki za hivi karibuni lakini leo Jumapili, Umoja wa Mataifa unaonekana kuwa na wasiwasi zaidi kuliko hapo awali. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anasema "ana wasiwasi sana".

Naibu wake wa Masuala ya Kibinadamu pia ameshtushwa kwenye mtandao wa kijamii wa X: Martin Griffiths anazungumza kuhusu kuongezeka kwa mapigano karibu na El Fasher. Lakini ni mjumbe wake kwa Sudan ambaye ndiye sahihi zaidi. Raia huyu wa Cameroon, Clémentine Nkweta-Salami, anaeleza kuhusu “Silaha nzito zinatumiwa kwa mapigano hayo. Mashambulizi katika maeneo yenye watu wengi katikati na mazingira ya El Fasher." yanasababisha “waathiriwa wengi,” anasema ofisa huyo wa Umoja wa Mataifa. "Raia waliojeruhiwa wanakimbizwa katika hospitali ya El Fasher" huku wengine "wanaojaribu kukimbia wamenaswa katika mapigano makali."

Clémentine Nkweta-Salami anatoa wito kwa "wahusika wote kujitenga na mji huo" ambapo kati ya watu 800,000 na milioni mbili wanaishi - vyanzo vinatofautiana kwa sababu El Fasher katika miezi ya hivi karibuni ilipokea wakimbizi wengi wa ndani wanaokimbia mapigano na unyanyasaji wa kikabila ambao unaangamiza majimbo yote ya Darfur.

Huko El Fasher, wengi wa wakimbizi wa ndani sio Waarabu. Wanamgambo wa FSR wanaajiriwa kwa wingi kutoka makabila ya Waarabu. Wataalamu wengi na wanaharakati kutoka mashirika ya kiraia ya Sudan wanaonyesha katika muktadha huu hofu yao kubwa ya umwagaji damu mpya, hasa kwa kuzingatia kile kilichotokea mwaka jana huko El Geneina, mji mdogo zaidi, mji mkuu wa Darfur Magharibi.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, kati ya Massaali 10,000 na 15,000 waliuawa kwa umati mnamo mwezi wa Juni 2023, jijini na barabarani ambako walikuwa wakilekea nchi jirani ya Chad, umbali wa kilomita 10 tu. Lakini Chad iko mbali na El Fasher na barabara zote zimefungwa na FSR, hivyo basi wasiwasi mkubwa umetanda Jumapili hii. Hata hivyo, ni lazima kusisitizwa kwamba haijulikani iwapo kushadidi huku kwa mapigano ni mwanzo au la kwa mashambulizi haya makubwa dhidi ya jiji hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.