Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Kumi na moja waangamia katika mashambulizi mawili ya waasi Beni, mashariki mwa DRC

Watu zaidi  10 wameuawa kikatili Jijini Beni Katika kata la Sayo, kilomita 10 na katikati mwa Jiji la Beni magaribi mwake. Duru za kiusalama mzimehusisha waasi wa Uganda wa ADF na washirika wao kwa mauaji hayo.

Mashirika ya kiraia katika eneo la Matembo wananyooshea lawama vikosi vya usalama na ulinzi kwamba vilionywa mara kadhaa kuhusu hatari inayosababishwa na uwepo wa waasi katika eneo hilo kwa wiki tatu zilizopita.
Mashirika ya kiraia katika eneo la Matembo wananyooshea lawama vikosi vya usalama na ulinzi kwamba vilionywa mara kadhaa kuhusu hatari inayosababishwa na uwepo wa waasi katika eneo hilo kwa wiki tatu zilizopita. © Sébastien Kitsa Musayi / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maeneo ya Matembo na Sayo yalikumbwa na jinamizi la mauaji siku mbili mfululizo siku ya Jumamosi na Jumapili, ambapo watu zaidi ya kumi waliuawa, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama.

Kulingana na tovuti ya Deutsche Welle, (DW) likinukuu asisa wa eneo la Matembo, watu sita waliuawa katika eneo hilo siku ya Jumamosi usiku, ambapo waasi wanaoshukiwa kuwa wa ADF waliendesha shambulio lao la kwanza.

Baada ya shambulio hilo, waasi hao walivamia kijiji cha Sayo na kuua watu wengine watano, na hivyo kufanya idadi ya waliouawa kufikia kumi na moja.

Afisa wa mji wa Beni Makofi Bukuku ameliambia shirika la habari la AFP kuwa idadi ya vifo katika eneo la Sayo huenda ikaongezeka, kwa sababu waasi bado wako katika eneo hilo.

Mashirika ya kiraia katika eneo la Matembo wananyooshea lawama vikosi vya usalama na ulinzi kwamba vilionywa mara kadhaa kuhusu hatari inayosababishwa na uwepo wa waasi katika eneo hilo kwa wiki tatu zilizopita. Jeshi la Kongo halijazungumzia mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.