Pata taarifa kuu
USALAMA-WAKIMBIZI

DRC: UNHCR inahitaji zaidi ya dola milioni 200 kuwasaidia waliokimbia makazi yao

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Wakimbizi (UNHCR) inahitaji zaidi ya dola za Kimarekani milioni 200 ili kukidhi mahitaji ya watu waliolazimika kutoroka makaazi yao mashariki mwa DRC.

Takriban watu 200,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano mapya katika maeneo ya Rutshuru na Masisi, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.
Takriban watu 200,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano mapya katika maeneo ya Rutshuru na Masisi, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Mwakilishi wa UNHCR nchini DRC Angele Dikongue Atangana ameayasema hayo hivi pundi Jumanne jioni Machi 12 mjini Kinshasa, wakati wa mkutano wa kwanza wa mwaka huu ulioandaliwa kwa ajili ya mabalozi wa nchi za kigeni nchini DRC.

“Niliwasisitizia wafadhili kuwa tunawashukuru sana kwa kile wanachofanya kutuunga mkono, katika kazi tunazofanya, lakini kuna nafasi ya kufanya zaidi. Kwa sababu kwa bahati mbaya hali si nzuri. Na kama njia ya mwisho, niliwaambia kwa kuzingatia mahitaji haya yote yanayokua, kwa upande wa mahitaji ya kibinadamu, tunahitaji zaidi ya dola milioni 200 za Kimarekani. Mwaka jana tulifikia kwa shida asilimia 50 ya ufadhili. Kwa hivyo asilimia 50 ya ufadhili ni chini ya kile tunachopaswa kuwa na uwezo wa kufanya kwa watu wanaoteseka,” amesema.

Lengo la mkutano huu lilikuwa kuwasilisha habari za hivi punde kutoka kwa shirika hili la Umoja wa Mataifa na kutetea ushirikiano wa hali ya juu kati ya washikadau wote ili kukidhi mahitaji ya watu waliolazimika kuyahama makaazi yao nchini DRC.

"Ni muhtasari ambao ni wa kisheria, mkutano wa kila robo mwaka ambao tunakuwa na wafadhili wetu na washirika wetu kwa ujumla, ili kuripoti kwao juu ya kile kinachotokea mashinani, huko tulipo haswa Mashariki mwa DRC. Na kwa shughuli zote za UNHCR nchini,” ameongezaAngele Dikongue Atangana.

Kulingana na Radio OKAPI mwakilishi huyo wa UNHCR nchini DRC pia ametoa wito wa kukomeshwa kwa uhasama na kurejea kwa amani mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.