Pata taarifa kuu

Sudan: Baraza kuu la usalama la UN lataka kusitishwa kwa vita wakati wa Ramadhan

Nairobi – Baraza kuu la usalama katika Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Sudan katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadan.

Aidha pande zinazopigana zimetakiwa kuruhusu ufikiaji wa misaada ya kibinadamu kwa walengwa bila ya kuwepo kwa vikwazo vyovyote
Aidha pande zinazopigana zimetakiwa kuruhusu ufikiaji wa misaada ya kibinadamu kwa walengwa bila ya kuwepo kwa vikwazo vyovyote © Brendan McDermid / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Aidha baraza hilo limesema hatua hiyo ya kusitishwa kwa vita pia itahakikisha raia milioni 25 wanaohitaji chakula wataweza kufikiwa na msaada.

Nchi 14 kwenye baraza hilo lenye wanachama 15 siku ya Ijumaa ziliunga mkono azimio lililopendekezwa na Uingereza, huku Urusi pekee ikisusia kupiga kura ambayo ilizitaka pande zote kwenye mzozo kutafuta suluhu ya mzozo huo kwa njia ya mazungumzo.

Mapigano yamekuwa yakiendelea nchini Sudan tangu Aprili 15, 2023, yakihusisha jeshi la Jenerali Abdel Fattah al-Burhan dhidi ya wanajeshi (RSF) wake Jenerali Mohamed Hamdan "Hemedti" Dagalo.

Idadi kubwa ya raia wa Sudan wanahitaji chakula cha msaada kutokana na mapigano yanayoendelea.
Idadi kubwa ya raia wa Sudan wanahitaji chakula cha msaada kutokana na mapigano yanayoendelea. REUTERS - EL TAYEB SIDDIG

Makumi ya maelfu ya watu wameuawa tangu wakati huo, milioni 8.3 wamelazimika kuyahama makazi yao na mapigano hayo yameharibu miundombinu na kudumaza uchumi.

Naibu balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa, James Kariuki, alitoa wito kwa pande hasimu kufanyia kazi wito wa UN unaolenga kumaliza mapigano.

Azimio hilo lilizitaka pande zote kusitisha uhasama mara moja kabla ya Ramadhani.

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan,amekuwa akipambana na vikosi vya naibu wake za zamani Hamdan Dagalo
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan,amekuwa akipambana na vikosi vya naibu wake za zamani Hamdan Dagalo AP - Marwan Ali

Aidha pande zinazopigana zimetakiwa kuruhusu ufikiaji wa misaada ya kibinadamu kwa walengwa bila ya kuwepo kwa vikwazo vyovyote.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Alhamisi alisema pande zote mbili zinapaswa kuheshimu maadili ya Ramadhani kwa kuheshimu usitishaji wa uhasama wakati wa Ramadhani huku akionya kwamba mzozo huo unatishia umoja wa Sudan na unaweza kuchochea hali ya kukosekana kwa utulivu wa kikanda kwa kiwango kikubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.