Pata taarifa kuu

Wanawake wanavyokabiliwa na mzigo wa magonjwa yasioambukiza

Nairobi – Wakati huu dunia, ikiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake, wanawake katika nchi zinazoendelea wanalazimika kubeba mzigo mkubwa wa kuwa walezi wa watu kwenye jamii hasa wanaougua magonjwa yasiyoambukizwa ambayo husababisha vifo vya watu milioni 41 duniani kwa mujibu wa shirika la afya, WHO.

Magonjwa haya ni  kama vile kisukari ,saratani , shinikizo la damu,kiharusi na magonjwa ya moyo.
Magonjwa haya ni kama vile kisukari ,saratani , shinikizo la damu,kiharusi na magonjwa ya moyo. REUTERS - Regis Duvignau
Matangazo ya kibiashara

Kufikia mwaka 2030,asilimia 74 ya vifo duniani vitakuwa vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza ,asilimia zaidi ya sabini vikichangiwa na mataifa yanayoendelea.

Idadi  hii kubwa ya wagonjwa wanaougua magonjwa haya,linawalazimu  wanawake wengi kuwa walezi.

Jenniffer Birir kutoka kaunti ya Bomet amekuwa akihudumia mgonjwa wa kisukari.

"Ukiwa na mgonjwa, hakuna mahali pakwenda, unamhudumia tu kila wakati." alieleza Jenniffer Birir.

00:17

Jenniffer Birir kutoka kaunti ya Bomet

Naya Samantha Onyanzwa akitokea kaunti ya Butere, anaelezea masaibu yake kabla mamake mzazi kufariki kutokana na kisukari na shinikizo la damu.

"Alikuwa na shinikizo la damu, tatizo la sukari na tatizo la moyo na wakati alipolazwa ilibidi nitoe muda wangu kumhudumia." alieleza Samantha Onyanzwa.

00:29

Samantha Onyanzwa kutoka kaunti ya Butere

Getrude Mbeyu muuguzi wa wagonjwa wa saratani Pwani ya Kenya ,anasema kupunguza mzigo huu ,sharti serikali za Afrika kuwekeza katika taasisi za kuwatunza wagonjwa wanaougua kwa muda mrefu.

"Serikali iwekeze zaidi katika kutoa mafunzo kwa wauguzi na hata kuwaajiri." alisema Getrude Mbeyu muuguzi wa wagonjwa wa saratani Pwani ya Kenya.

00:07

Getrude Mbeyu muuguzi wa wagonjwa wa saratani Pwani ya Kenya

Magonjwa haya ni  kama vile kisukari ,saratani , shinikizo la damu,kiharusi na magonjwa ya moyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.