Pata taarifa kuu

Fidia ya kwanza kwa waathiriwa wa dikteta wa zamani wa Chad Hissène Habre

Zaidi ya waathiriwa 10,000 au jamaa wa waathiriwa wa dikteta wa zamani wa Chad Hissène Habre wameanza kupokea fidia kutoka kwa serikali, miaka minane baada ya kifungo chake cha maisha kwa uhalifu dhidi ya binadamu, mashirika yasiyo ya kiserikali yametangaza siku ya Jumanne.

Hissène Habré akizungukwa na askari baada ya kusikilizwa mahakamani, Julai 2, 2013 huko Dakar.
Hissène Habré akizungukwa na askari baada ya kusikilizwa mahakamani, Julai 2, 2013 huko Dakar. © AFP/Stringer
Matangazo ya kibiashara

"Malipo yalianza Februari 23," inabaini Tume ya Kimataifa ya Wanasheria (ICJ) katika taarifa kwa vyombo vya habari, ambayo inabainisha kuwa fidia ya FCFA bilioni 10 (takriban euro milioni 15.2) inalenga "waathirika wa magereza na (kwa) familia za wale waliouawa chini ya utawala wa Habre.” Dikteta huyo wa zamani, aliyepinduliwa mwaka 1990 nchini Chad, aliaga dunia akiwa gerezani huko Dakar mnamo Agosti 24, 2021.

"Kuna takriban waathirika 10,800, kila mmoja alipata FCFA 925,000 (euro 1,410). Tuligawana kwa usawa, waathiriwa wa moja kwa moja na wasio wa moja kwa moja walipokea kiasi sawa," rais wa Chama ameliambia shirika la habari la AFP.

Kiasi hiki, hata hivyo, kingewakilisha tu "sehemu ndogo ya kile walichopewa na mahakama, na kiasi, kidogo zaidi ya kile wanachostahili kupata chini ya sheria za kimataifa", imesema ICJ. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inakumbusha haswa kwamba mahakama ya Rufaa ya mahakama ya haki Afrika huko Dakar, mahakama maalum inayoungwa mkono na Umoja wa Afrika (AU) ambayo ilimtia hatiani Habre, ilitoa mwezi Aprili 2017 faranga za CFA bilioni 82 (euro milioni 125) kwa waathirika.

Mahakama hii, ambayo ilithibitisha kuhukumiwa kwa Hissène Habré mwaka wa 2017, pia iliagiza Wizara ya Fedha ya AU kuwafidia waathiriwa kutokana na mali na michango ya hiari ya kiongozi huyo wa zamani. Lakini hazina hii bado haifanyi kazi huku waathiriwa wengi wakifariki bila kupokea chochote.

Mnamo Machi 2015, vyombo vya sheria vya Chad vilikuwa tayari vimewahukumu maafisa 24 wa zamani wa polisi wa kisiasa chini ya utawala wa Habre kulipa fidia ya FCFA bilioni 75 (euro milioni 114) kwa waathiriwa waliotambuliwa, na kuamuru serikali kulipa nusu ya kiasi hicho na waliopatikana na hatia kulipa kiasi kingine.

Hissène Habré, ambaye aliongoza Chad kutoka mwaka 1982 hadi mwaka 1990 na ambaye alipata hifadhi nchini Senegal baada ya kuondolewa madarakani, alikamatwa, kushtakiwa na kuhukumiwa na mahakama hii maalum. Alipatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu, ubakaji, mauaji, utumwa na utekaji nyara na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kufuatia kesi ambayo haijawahi kushuhudiwa.

Tume ya uchunguzi ya Chad iliweka idadi ya waathiriwa wa ukandamizaji chini ya utawala wa Habre kuwa 40,000. Dikteta huyo wa zamani alitumikia kifungo chake nchini Senegal ambapo alikufa kwa UVIKO mnamo mwezi wa Agosti 2021 akiwa na umri wa miaka 79 na ambapo alizikwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.