Pata taarifa kuu

DRC yalaani mkataba wa ushirikiano kati ya Rwanda na EU kuhusu malighafi

Mkataba wa ushirikiano kuhusu malighafi uliotiwa saini kati ya Rwanda na Umoja wa Ulaya (EU) mnamo Februari 19, 2024 umekosolewa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). DRC inalaani uporaji wa madini ya Kongo kwa zaidi ya miaka 20 na baadhi ya mataifa ya kigeni, ikiwa ni pamoja na Rwanda. Kwa upande wa EU, Brussels inatetea makubaliano haya na inakumbusha kuwa imelaani mara nyingi tabia ya wahusika mbalimbali kwa makundi yenye silaha mashariki mwa DRC.

Bendera za Umoja wa Ulaya zikipepea mbele ya makao makuu ya Tume ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji.
Bendera za Umoja wa Ulaya zikipepea mbele ya makao makuu ya Tume ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. © Yves Herman / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), makubaliano ya ushirikiano kuhusu malighafi yaliyotiwa saini kati ya Rwanda na Umoja wa Ulaya (EU) yanazua sintofahamu, anaripoti mwandishi wetu mjini Goma, Coralie Pierret. Tangu kutiwa saini kwake Februari 19, 2024, misimamo dhidi ya mkataba huu imeongezeka na kukemea uporaji wa madini ya Kongo kwa zaidi ya miaka 20 na baadhi ya nchi za kigeni, ikiwa ni pamoja na Rwanda. Jeshi la Rwanda, ambalo pia linashutumiwa na nchi kadhaa za Maghatribi na Umoja wa Mataifa, kwa kushiriki katika uvunjifu wa amani mashariki mwa DRC na kuwa na wanajeshi katika ardhi ya Kongo kuwaunga mkono waasi wa M23.

Ilikuwa Lucha, Februari 21, 2024, ambayo ilifungua mpira wa maazimio. Katika barua hiyo, vuguvugu la raia limekasirishwa "na msaada usio na masharti ambao Umoja wa Ulaya hutoa kwa Rwanda".

"Udongo wa chini wa Rwanda haujajaa madini haya"

Mwanzoni mwa wiki, mpango wa uwekezaji wa Ulaya kwa malighafi ulitiwa saini mjini Kigali. Mkataba kama huo wa maelewano ulihitimishwa kati ya EU na DRC mwezi Oktoba mwaka uliyopita. Lengo hasa ni "kukuza ujuzi katika sekta ya madini na kuboresha uwazi na ufuatiliaji". Hii inahusu hasa tantalum na niobium, metali mbili zinazoitwa coltan, mkakati wa utengenezaji wa teknolojia za kisasa zikiwemo simu mahiri na kompyuta.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Kongo pia haijakata tamaa, kupitia taarifa kwa vyombo vya habari ya Februari 21: "Serikali inatarajia kutoka kwa mamlaka ya Umoja wa Ulaya ufafanuzi wa tabia hii isiyoeleweka wakati wanaendelea kuthibitisha nia yao ya kuchangia kumalizika kwa usalama. mgogoro wa Mashariki mwa Kongo pamoja na unyonyaji haramu wa maliasili zake. "

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2018, raia wa Kongo Denis Mukwege, anakumbusha kwamba mzozo wa mashariki mwa DRC ni wa kiuchumi na kwamba unyonyaji au biashara haramu ya madini inatambuliwa kama sababu kuu ya ghasia.

Kwa upande wake, EU inakanusha nia yoyote mbaya kwa upande wake, anaripoti mwandishi wetu wa Brussels, Pierre Benazet. Unathibitisha manufaa ya makubaliano hayo, huku ukilaani hatua ya makundi yenye silaha mashariki mwa DRC.

"Umoja wa Ulaya daima ni muigizaji mwenye malengo," tume hiyo ilijibu Februari 22. Kulingana na Peter Stano, msemaji wa Josep Borrell, mkuu wa diplomasia ya Ulaya, EU "haichukui upande", imekuwa na mtazamo wa usawa kila wakati, umelaani mara nyingi tabia ya wadau mbalimbali huku ukilaani makundi yenye silaha mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.