Pata taarifa kuu
MTAZAMO-USALAMA

Mapigano mashariki mwa DRC: Kwa nini udhibiti wa mji wa Sake ni wa kimkakati

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), katika siku za hivi karibuni kumetokea mapigano kati ya jeshi la Kongo wakisaidiwa na wanamgambo wa eneo hilo, Wazalendo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda. mji ulioko takriban kilomita ishirini magharibi mwa Goma na kuchukuliwa kuwa kizuizi cha kimkakati kwenye barabara ya kuelekea mji mkuu wa mkoa.

[Image d'illustration] Des personnes se rassemblant à côté de véhicules de la Force de défense nationale sud-africaine (SANDF) dans le cadre de la mission de la Communauté de développement de l'Afriqu
Watu wakikusanyika karibu na magari ya jeshi la ulinzi wa taifa la Afrika Kusini (SANDF) kama sehemu ya ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walipokuwa wakikimbia eneo la Masisi kufuatia mapigano kati ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali, kwenye barabara karibu na Sake mnamo Februari 7, 2024. AFP - AUBIN MUKONI
Matangazo ya kibiashara

 

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), milio ya risasi ya hapa na pale ilisikika siku ya Jumatano, Februari 14 karibu na mji wa Sake, katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Mapigano kati ya jeshi la Kongo, likisaidiwa na wanamgambo wa ndani, Wazalendo, na waasi wa M23, wakiungwa mkono na jeshi la Rwanda.

Katika siku kumi zilizopita, hali ya usalama imezorota kwa kiasi kikubwa: waasi - waliopo katika eneo hilo kwa miezi kadhaa - wameanzisha mashambulizi mapya huko Sake na viunga vyake.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, vuguvugu la waasi pia lilithibitisha kuwa lilitaka kuuteka mji huo ulioko takriban kilomita ishirini magharibi mwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini. Kwa nini Sake? Je, mji huu una mkakati gani?

Sake, eneo la kimkakati katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Sake, eneo la kimkakati katika mkoa wa Kivu Kaskazini. © Studio graphique FMM

Sake ni mji wa njia panda: ni kutoka hapo ndipo barabara kuu tatu zinaondoka: kuelekea kaskazini, barabara inayoelekea Butembo; kuelekea magharibi, ambayo inaelekea Masisi Center na Walikale; na kuelekea kusini, kwenda Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini.

Barabara mbili za kwanza zilikatwa na M23 wiki chache zilizopita, na kutatiza usambazaji wa bidhaa za chakula kwa Goma.

Maharage, mihogo, viazi, maziwa: bidhaa kaskazini mashariki mwa eneo la Masisi na kusafirishwa hadi Goma, kwa lori, magari au pikipiki.

Mhimili wa tatu, unaoelekea kusini kuelekea Minova, Bukavu, ulizuiliwa wiki iliyopita, na kutekwa kwa Shasha na waasi, wilaya iliyoko kwenye mwambao wa Ziwa Kivu. Huko pia, barabara hii ilitumiwa kusafirisha ndizi na sombé, zilizovunwa kusini mwa eneo la Masisi, hadi Goma.

Kuzingira, kutenga Goma

Kutekwa kwa Saké kwa hivyo ni kimkakati: inahusisha kuzinigira na kutenga zaidi mji wa Goma, jiji lenye karibu milioni 2 ya wakaazi.

Hasa kwa vile barabara kutoka mji mkuu wa mkoa kuelekea kaskazini ilikuwa tayari imekatizwa mara kwa mara kwa karibu miaka miwili na uwepo wa M23 katika eneo hili, katika maeneo ya Nyiragongo na Rutshuru.

Pamoja na athari: kwenye masoko ya Goma, baadhi ya bidhaa  zinazidi kuwa nadra. Lakini, juu ya yote, bei za vyakula zimepanda. Wiki chache zilizopita, viazi vitamu vitano viliuzwa kwa faranga 1,000 za Kongo. Leo, ni mara mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.