Pata taarifa kuu

WFP yataka uwezo zaidi kusaidia mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao DRC

Kutokana na ukosefu wa uwezoo wa kutosha, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema siku ya Ijumaa mjini Kinshasa kuwa nlimesikitishwa na kuona linaweka kikomo cha msaada wake kwa watu waliokimbia makazi yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambao wanafikia zaidi ya milioni sita, hasa Mashariki.

Kutokana na "uhaba wa fedha", WFP lazima "itangulize msaada", na kuwaacha mamilioni ya watu bila msaada wa chakula, imesema taarifa hiyo. "Tunatoa mgao kamili kwa watu walioathirika zaidi (...) badala ya kutawanya misaada kupita kiasi," anaelezea Natasha Nadazdin, naibu mkurugenzi wa WFP nchini DRC, katika taarifa.
Kutokana na "uhaba wa fedha", WFP lazima "itangulize msaada", na kuwaacha mamilioni ya watu bila msaada wa chakula, imesema taarifa hiyo. "Tunatoa mgao kamili kwa watu walioathirika zaidi (...) badala ya kutawanya misaada kupita kiasi," anaelezea Natasha Nadazdin, naibu mkurugenzi wa WFP nchini DRC, katika taarifa. AP - Robert Bumstead
Matangazo ya kibiashara

 

WFP "inahitaji dola milioni 397 kwa dharura kutoa msaada muhimu wa chakula mashariki mwa DRC katika kipindi cha miezi sita ijayo, kusaidia watu milioni 1.5 waliopewa kipaumbele," shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaandika katika taarifa. Linahitaji "jumla ya dola Milioni 543 ili kuendelea na shughuli kote nchini," taarifa hiyo inaongeza.

Mashariki mwa Kongo, hasa mikoa mitatu ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, yamekumbwa na ghasia kwa kutumia silaha kwa takriban miaka 30. Huko Kivu Kaskazini, kuibuka tena miaka miwili iliyopita kwa uasi wa M23 ("March 23 Movement"), wanaosaidiwa na nchi jirani ya Rwanda kulingana na ripoti mbalimbali na serikali ya DRC, kulizidisha hali mbaya ya kibinadamu ambayo tayari ilikuwa mbaya.

Kutokana na "uhaba wa fedha", WFP lazima "itangulize msaada", na kuwaacha mamilioni ya watu bila msaada wa chakula, imesema taarifa hiyo. "Tunatoa mgao kamili kwa watu walioathirika zaidi (...) badala ya kutawanya misaada kupita kiasi," anaelezea Natasha Nadazdin, naibu mkurugenzi wa WFP nchini DRC, katika taarifa.

"Ni uamuzi mgumu, ndiyo maana tunahitaji fedha kwa haraka," anasisitiza kmuu huyo wa WFP nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.