Pata taarifa kuu

Bunge la Kitaifa: Kikao cha uzinduzi cha bunge la 4 kufanyika Jumatatu hii

Wabunge wapya wa kitaifa waliochaguliwa katika uchaguzi wa Desemba 20, 2023 wameitishwa Jumatatu hii, Januari 29 katika makao makuu ya Baraza la Wawakilishi, mjini Kinshasa katika kikao cha uzinduzi kitakachongozwa na Katibu Mkuu wa Bunge kwa mujibu wa ibara ya 114 ya Katiba.

Makao makuu ya Baraza la Bunge la taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mjini Kinshasa, Februari 2, 2023.
Makao makuu ya Baraza la Bunge la taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mjini Kinshasa, Februari 2, 2023. © Alexis Huguet / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Mjadala huu utafuatiwa na uanzishwaji wa afisi ya umri itakayoongozwa na mbunge mwenye umri mkubwa kuliko wote wanaounda bunge la taifa, akisaidiwa na wabunge wawili wenye umri mdogo zaidi.

Ofisi hii ya umri itaendesha kikao hiki cha uzinduzi hadi ajenda itakapokwisha.

Chini ya kifungu cha 114 cha katiba, afisi ya muda itaongozwa na mbunge mwenye umri mkubwa zaidi kuliko wabunge wote , ambaye anashukiwa kuwa Christophe Mboso Nkodia, akisaidiwa na wabunge wawili wenye umri mdogo zaidi akiwemo Emmanuel Bahati, mtoto wa rais wa sasa wa Bunge la Seneti.

Ofisi hii mpya itaunda tume maalum ambayo itathibitisha faili za kila mbune kwa nia ya uthibitisho ujao wa mamlaka yao.

Hii itahusisha, kwa mujibu wa ibara ya 108 ya Katiba, kujiuzulu kwa wajumbe kadhaa wa Serikali na taasisi nyingine za nchi kwa sababu za kutowiana kwa majukumu.

Miongoni mwao, kuna hasa: Waziri Mkuu Sama Lukonde, Naibu Waziri Mkuu Vital Kamerhe, Peter Kazadi, Christophe Lutundula pamoja na mawaziri kadhaa waliochaguliwa kuwa wabunge.

Rais wa sasa wa Seneti Modeste Bahati Lukwebo na wajumbe wa afisi yake pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi za mikoa pia watalazimika kujiuzulu ili mamlaka zao ziwe kuidhinishwa.

Bado kwa mujibu wa ibara ya 114 ya Katiba, kikao hiki cha uzinduzi kitaendelea pia kwa maendeleo ya kanuni za ndani za Bunge, na kufuatiwa na kuwekwa kwa ofisi ya mwisho itakayoashiria kufungwa kwa kikao hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.