Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Uchaguzi wa urais nchini Senegal: wagombea 20 waidhinishwa, Karim Wade aondolewa

Baraza la Katiba la Senegal lilichapisha siku ya Jumamosi orodha ya mwisho ya wagombea 20 kwa uchaguzi wa urais wa Februari 25, ambao haujumuishi Karim Wade, mtoto wa kiume na waziri wa Rais wa zamani Abdoulaye Wade, shirika la habari la AFP limebainisha.

Baraza la Katiba (Mahakama ya Katiba) la Senegal limeidhinisha wagombea ishirini kwa uchaguzi wa urais.
Baraza la Katiba (Mahakama ya Katiba) la Senegal limeidhinisha wagombea ishirini kwa uchaguzi wa urais. William de Lesseux/RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Orodha hiyo inajumuisha mgombea wa kambi ya urais, Waziri Mkuu Amadou Bâ, wakuu wa zamani wa serikali na wapinzani Idrissa Seck na Mahammed Boun Abdallah Dionne, meya wa zamani wa Dakar Khalifa Sall na Bassirou Diomaye Diakhar Faye, aliyetangazwa kama mgombea mbadala wa mpinzani anayefungwa Ousmane Sonko.

Bw. Faye, 43, mwanachama wa chama kilichovunjwa cha Bw. Sonko, pia anazuiliwa, lakini bado hajahukumiwa.

Ousmane Sonko, kiongozi mkuu katika mvutano uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili na Serikali, hali ambayo ilizua matukio kadhaa ya machafuko mabaya, haonekani kwenye orodha, kama ilivyotarajiwa. Ousmane Sonko, ambaye ni maarufu miongoni mwa vijana, alikuwa miongoni mwa wagombea wanaopewa nafasi zaidi ya kushinda katika uchaguzi huo wa urais.

Alipatikana na hatia mnamo mwezii wa Juni ya unyanyasaji wa kingono kwa msichana mdogo na kuhukumiwa miaka miwili jela, alifungwa gerezani mwishoni mwa mwezi Julai kwa mashtaka mengine, ikiwa ni pamoja na kutoa wito wa kuanzisha kwa uasi, kusirikiana na wahalifu wenye uhusiano na ugaidi na jaribio la kuhatarisha usalama wa serikali.

Bw. Sonko alilaani njama ya kumzuia kushiriki katika uchaguzi wa urais wa Februari 2024, jambo ambalo serikali inakanusha.

Rais Macky Sall, aliyechaguliwa mwaka wa 2012 kwa miaka saba na kuchaguliwa tena mwaka wa 2019, alitangaza mwezi wa Julai kwamba hatagombea tena uchaguzi Februari 2024. Mwezi wa Julai 2023 alimchagua Waziri Mkuu Amadou Bâ kumrithi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.