Pata taarifa kuu

Maofisa wa jeshi la maji la Marekani waripotiwa kutoweka pwani ya Somalia

Nairobi – Wanajeshi wawili wa jeshi la Maji la Marekani wameripotiwa kutoweka baharini walipokuwa wakiendesha operesheni katika pwani ya Somalia kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la nchi hiyo.

Washington imeliorodesha kundi la Al-Shabaab kama shirika la kigaidi
Washington imeliorodesha kundi la Al-Shabaab kama shirika la kigaidi REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Maofisa hao wawili waliripotiwa kutoweka siku ya Alhamisi jioni kama ilivyothibitisha kamandi kuu ya Marekani katika taarifa fupi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa sasa shughuli za utafutaji na uokoaji zinaendelea ili kuwapata mabaharia hao wawili.

Wanajeshi wa Marekani wamekuwa wakifanya kazi nchini Somalia kwa muda mrefu kwa uratibu wa serikali ambapo yamekuwa yakitekeleza mashambulio ya angani kwa ushirikiano na jeshi la Somalia katika vita vyake dhidi ya waasi wenye itikadi kali wa Al-Shabaab.

Washington imeliorodesha kundi la Al-Shabaab kama shirika la kigaidi na kwamba ni mtandao mkubwa unaofanya kazi na kundi la kigaidi la Al-Qaeda duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.