Pata taarifa kuu

Cape Verde, nchi ya 3 barani Afrika kutokomeza Malaria

Cape Verde, kisiwa kinachopatikana katika Bahari ya Atlantiki, imekuwa nchi ya tatu barani Afrika ambako ugonjwa wa Malaria unachukuliwa kuwa umetokomezwa rasmi huku ugonjwa huo ukiendelea kuua mamia kwa maelfu ya watu barani humo kila mwaka, limesema Shirika la Afya Duniani, WHO.

Hatua hii imetajwa kuwa mafanikio katika vita dhidi ya malaria
Hatua hii imetajwa kuwa mafanikio katika vita dhidi ya malaria © UNICEF
Matangazo ya kibiashara

Cape Verde, nchi yenye wakazi wapatao 500,000, baada ya Mauritius mwaka 1973 na Algeria mwaka 2019, imekuwa nchi ya tatu barani Afrika inayotambuliwa na WHO kama imetokomeza kabisa Malaria. WHO inazungumza katika taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu "mafanikio makubwa yaliyopigwa katika afya ya kimataifa".

Zaidi ya nchi 40 zimmepata cheti kama hicho, kinachotolewa wakati nchi inatoa ushahidi kwamba mlolongo wa maambukizi ya mbu wa kaya umekatizwa katika ngazi ya kitaifa kwa angalau miaka mitatu mfululizo.

Malaria, hata hivyo, inaendelea kusababisha vifo vya takriban watu 608,000 mwaka 2022, huku kukiwa na maambukizi karibu milioni 250 duniani kote, inasema tovuti ya WHO. Nchi 50 za Afrika zina idadi kubwa ya vifo, zikiwa na vifo 580,000, au 95% ya jumla ya kimataifa, na 94% ya maambukizi. Watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano wanawakilisha 80% ya vifo barani Afrika.

"Mafanikio ya Cape Verde ni mwanga wa matumaini kwa kanda ya Afrika na kwingineko. Inadhihirisha kuwa kwa utashi thabiti wa kisiasa, sera madhubuti, ushirikishwaji wa jamii na ushirikiano wa sekta mbalimbali, kutokomeza malaria ni lengo linaloweza kufikiwa," amesema Dk Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa WHO katika kanda ya Afrika, akinukuliwa na shirika hilo.

Mafanikio haya, baada ya mengine, "yanatufanya tuwe na matumaini kwamba, kutokana na zana zilizopo au mpya, hasa chanjo, tunaweza kuanza kuwa na ndoto ya ulimwengu usio na Malaria", ameongeza Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Malaria huambukizwa kwa binadamu hasa kwa kuumwa na aina fulani za mbu jike walioambukizwa na hutokea hasa katika nchi za Tropiki. Inaweza pia kuambukizwa kwa njia ya kuongezewa damu na sindano zilizoambukizwa. Inaweza kuwa kidogo, ikiwa na dalili kama vile homa na maumivu ya kichwa, lakini pia inaweza kusababisha kifo ndani ya saa 24 na vimelea vya P. falciparum, ambavyo hupatikana zaidi barani Afrika.

Mapambano dhidi ya malaria kwa muda mrefu yamekuwa yakihusisha hasa uzuiaji kwa kutumia vyandarua au unywaji wa dawa za kujikinga na matumizi ya dawa za kuua wadudu. Walakini, WHO inaandika kwenye wavuti yake kupendekeza chanjo mbili tangu 2021.

WHO inaangazia faida iliyopata Cape Verde kutokana na kutokomeza Malaria. "Hii inaweza kuvutia wageni zaidi na kukuza shughuli za kijamii na kiuchumi katika nchi ambayo utalii unawakilisha karibu 25% ya Pato la Taifa," anasema.

WHO inakumbuka kwamba kabla ya miaka ya 1950, visiwa hivyo vilikumbwa na magonjwa ya mlipuko mara kwa mara na kwamba visiwa vyote viliathiriwa. Nchi ilifanikiwa kumaliza ugonjwa huo mnamo 1967 na 1983 kupitia kunyunyizia dawa, lakini makosa yaliyofuata yalisababisha ugonjwa huo kurudi. Tangu kilele cha mwisho mwishoni mwa miaka ya 1980, Malaria ilibakia katika visiwa viwili tu, Santiago na Boa Vista, inasema WHO.

Kutokomeza Malaria kulikua lengo la afya la kitaifa nchini Cape Verde mwaka 2007 na kusababisha mpango mkakati kati ya mwaka 2009 na 2013, shirika hilo limesema. WHO inataka uchunguzi uenee zaidi, matibabu ya mapema na huduma ya bure kutolewa kwa wageni. Cape Verde imedumisha umakini licha ya janga la Uviko-19, WHO imepongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.