Pata taarifa kuu

Sudan: Makabiliano kati ya jeshi na RSF yanaendelea kuripotiwa

Nairobi – Nchini Sudan, mapigano kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF, katika mji mkuu Khartoum, yamesababisha vifo vya raia 33, kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la wanasheria wanaounga mkono demokrasia.

Mapigano ambayo yalizuka Aprili 15 jijini Khartoum, yamesabaisha vifo vya zaidi ya watu elfu 12 na 100, UN ikisema zaidi ya watu milioni 7 wamelazimika kuhama makazi yao
Mapigano ambayo yalizuka Aprili 15 jijini Khartoum, yamesabaisha vifo vya zaidi ya watu elfu 12 na 100, UN ikisema zaidi ya watu milioni 7 wamelazimika kuhama makazi yao REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo linasema raia 23 waliuawa hapo hapo jana huku wengine kadhaa wakijeruhiwa kufuatia mashambulio ya anga katika wilaya ya Soba, jijini Khartoum, shirika hilo likituhumu jeshi la serikali ambalo bado lina udhibiti wa anga.

Shirika hilo aidha, lilithibitisha vifo vya watu wengine 10 kutokanana mashambulio ya mizinga kusini mwa Khartoum.

Mapigano hayo yameenea hadi maeneo ya kusini mwa nchi hiyo, na hivi karibuni yamefika katika jimbo la Al-jazira ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekimbilia kutafuta hifadhi.

Haya yanajiri wakati huu kukiwa na jitihada za kikanda kuwakutanisha ana kwa ana majenerali wawili wanaopigana, Abdel Fattah al-Burhan na kiongozi wa RSF Mohamed Hamdan Daglo.

Mapigano ambayo yalizuka Aprili 15 jijini Khartoum, yamesabaisha vifo vya zaidi ya watu elfu 12 na 100, UN ikisema zaidi ya watu milioni 7 wamelazimika kuhama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.