Sudan: Hamdan Daglo anatuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita
Nairobi – Kiongozi wa kikosi cha wanamgambo nchini Sudan cha RSF Mohamed Hamdan Daglo anatuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita nchini Sudan, wakati huu akiendeleza ziara yake kwa mataifa ya Kikanda, ziara inayondekana kuwagawa msimamo ya viongozi wa kikanda.
Imechapishwa:
Cheza - 00:59
Hamdan Daglo amekua akifanya safari za kikanda ikiwa ni juhudi za kujaribu kujaribu kutafuta ungwaji mkono na viongozi wa kikanda na bara Afrika, kujaribu kusuluhisha mzozo ambao umepelekea vita kati ya kikosi chake cha RSF na jeshi la Sudan.
Hamdan amefanya mazungmzo na marais wa Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Rwanda, na Djibouti pamoja na Ethiopia, ili kutafta njia mwafaka ya kumaliza mzozo na kwamba mchakato wa amani unaoendelezwa na IGAD, unastahili kufikia suluhu ya kisiasa itakayoleta amani ya kudumu nchini humo, ambapo kiongozi huyo anapata ungwaji mkono kutoka utawala wa Chad.
Naye kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Sudan Abdel Fattah Al-Burhan akionekana kupata ungwaji mkono kutoka kwa Misri na Eritrea.
Hivi majuzi wapiganaji wa RSF nchini Sudan wameonesha utayari wao wa kusitisha mara moja mapigano na bila masharti yoyote kupitia mchakato wa mazungumzo na Jeshi la Sudan.
Vita nchini Sudan vilivyoanza mwezi Aprili mwaka jana, na tayari vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 12,000 huku Umoja wa Mataifa ukisema kuwa zaidi ya watu milioni 7 wameyakimbia makazi yao.
Tume ya umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, hapo jana ililaani vurugu zilizosababisha vifo vya raia 28 kwenye mji wa Duk, kaunti ya Jonglei.
UNMISS sasa inawataka viongozi wa eneo la Jonglei na Pibor, kukutana kwa mazungumzo ili kuepuka mashambulio ya ulipizaji kisasi baada ya vijana wa Murle kutekeleza mauaji hayo.