Pata taarifa kuu

Somalia 'yafuta' makubaliano ya kibiashara kati ya Ethiopia na Somaliland

Mvutano unaongezeka katika Pembe ya Afrika. Rais wa Somalia alitangaza Jumamosi jioni Januari 6 kwamba alitia saini sheria ya "kufuta" makubaliano ya kibiashara kati ya Ethiopia na eneo linalojitenga la Somaliland. Somaliland ilijitangaza kuwa huru kutoka kwa Somalia mwaka 1991, lakini haitambuliki na jumuiya ya kimataifa.

Mahali pa bandari ya Berbera, iliyoko katika eneo lililojitenga la Somaliland, Somalia.
Mahali pa bandari ya Berbera, iliyoko katika eneo lililojitenga la Somaliland, Somalia. © Studio FMM
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Albane Thirouard

Itifaki ya mkataba iliyotiwa saini kati ya Somaliland na Ethiopia, ambao ilitiwa saini Januari 1, unapaswa kutoa ufikiaji wa baharini kwa Addis Ababa, lakini Mogadishu inaiona kuwa "kinyume cha sheria" na kwenda kinyume na uhuru wake. "Sheria hii inaonyesha dhamira yetu ya kulinda umoja wetu, mamlaka yetu na uadilifu wa eneo letu," amesema Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud kwenye X (zamani ikiitwa Twitter). Sheria ambayo "imefuta" itifaki ya mkataba kati ya Addis Ababa na Hargeisa, ambayo anaiona kama "kinyume cha sheria", amesema rais wa Somalia.

Upeo wa sheria hii, hata hivyo, unaonekana kuwa wa mfano. Eneo lililojitenga la Somaliland limekuwa na serikali yake tangu 1991, inachapisha sarafu yake yenyewe na kutoa pasi zake za kusafiria. Ingawa Somalia inapinga vikali madai yake ya uhuru, kwa hakika ina udhibiti mdogo juu ya mambo ya eneo hilo lililojitangaza taifa huru. Ukosefu wa kutambuliwa kimataifa, hata hivyo, unaiweka Somaliland katika hali ngumu na kujikuta imetengwa kimataifa.

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini Januari 1 yananuia kuipa Ethiopia, nchi isiyo na bahari, ufikiaji wa kipande cha ardhi cha kilomita ishirini kwenye pwani ya Somaliland kwa kipindi cha miaka 50. Hargeisa ilidai kuwa kwa kubadilishana, Ethiopia ingeitambua rasmi Somaliland kama taifa huru. Addis Ababa haikuthibitisha hili, lakini ilionyesha katika taarifa kwamba "tathmini ya kina" itafanywa ili kuchukua msimamo.

Mara tu ilipotangazwa, itifaki ya mkataba ilikataliwa vikali na Mogadishu, ambayo ilishutumu "kitendo cha uchokozi".

Ongezeko hili la mivutano pia linatia wasiwasi jumuiya ya kimataifa. Marekani, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, lakini pia Umoja wa Nchi za Kiarabu, Misri na Uturuki wametoa wito wa kuheshimiwa kwa uhuru wa Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.