Pata taarifa kuu

Raia waitikia zoezi la upigaji kura licha ya matatizo ya kiufundi kujitokeza Lubumbashi

Zoezi la upigaji kura linaendelea mjini Lubumbashi. Jiji lina vituo 2,008 vya kupigia kura na vyote vinafanya kazi ingawa vingine vimepata matatizo ya kiufundi.

Wapiga kura wamehesabiwa katika orodha ya wapiga kura katika kituo cha kupigia kura katika shule ya Bwakya mjini Lubumbashi tarehe 20 Desemba 2023.
Wapiga kura wamehesabiwa katika orodha ya wapiga kura katika kituo cha kupigia kura katika shule ya Bwakya mjini Lubumbashi tarehe 20 Desemba 2023. AFP - PATRICK MEINHARDT
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na mwanahabari wetu huko Lubumbashi Denise Maheho,

Katika uwanja wa shule Banabii,  katika wilaya ya Katuba, mamia ya watu wamejipanga mbele ya vituo vya kupigia kura. Lakini mbele ya chumba F, kuan msongamano mkubwa wa watu, raia wakiwa na kadi zao za kupiga kura mikononi.

"Kwanza inabidi utafute jina lako kwenye daftari la wapiga kura. Baada ya hapo, unajipanga kwenye  mstari. Halafu wanakusanya kadi na kisha, maafisa wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) wataita majina. Sisi ndio tunaleta fujo.

Nao wawakilishi wa vyama vya siasa wana uzuni amesema Elizée mmoja wao

Kawaida sisi wawakilishi wa vyama vya siasa tunapashwa kupiga kura na baada ya hapo tunasalia ndani ya kituo ili kufuatilia jinsi mambo yanavyoendelea. Lakini hawaturuhusu

Katika shule ya Espoir, pia kunaripotiwa umati wa watu. Gustave ana huzuni. Hakupiga kura kwa sababu alikuwa amepata kadi yake huko Kolwezi, kilomita 300 kutoka Lubumbashi.

"Kama Mkongo, nina haki ya kupiga kura popote nilipo nchini. Nina uchungu kwa sababu sikuweza kupiga kura. Niliombwa nirudi pale nilipoandikishwa" , amesema Gustave.

Katika kituo kingine cha kupigia kura jirani, mjadala mkali ulibukaa. Maafisa wa polisi wamemkamata mtu ambaye aliendelea na kampeni ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.