Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi DRC: Umoja wa Ulaya watangaza kufuta misheni yake ya waangalizi

Umoja wa Ulaya umeamua kufuta ujumbe wake wa uangalizi wa uchaguzi nchini DRC katika hali yake ya awali. Umoja wa Ulaya unaeleza kuwa hii ni kutokana na vikwazo vya kiufundi vilivyo nje ya uwezo wake. Awali ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya ulifahamisha kuwa bado haujapewa vibali vyote vinavyohitajika vinavyowaruhusu kutumia vifaa vyake vya mawasiliano nchini DRC, ikiwa ni pamoja na simu na vifaa vya mtandao vya satelaiti.

Mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell mnamo Novemba 14, 2023 huko Brussels.
Mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell mnamo Novemba 14, 2023 huko Brussels. AP - Virginia Mayo
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi

Umoja wa Ulaya haukusubiri mkutano mpya uliopangwa kufanyika Jumatano hii mchana katika mji mkuu wa Kongo. Uamuzi huo umetolewa moja kwa moja na Josep Borell. Brussels inabaini kwamba imesubiri vya kutosha, amebaini mwanadiplomasia aliyeko Kinshasa.

Katika taarifa, EU inahimiza mamlaka ya Kongo na washikadau wote katika mchakato huu kuendelea na juhudi zao ili kuhakikisha kwamba raia wa Kongo wanaweza kutumia kikamilifu haki zao halali za kisiasa na kiraia wakati wa uchaguzi ujao. Kinshasa bado haijazungumzia chochote kuhusiana na uamuzi huu.

Ni ngumu katika hatua hii kubaini athari ya hatua kama hiyo. "Ni hali tete. Katika hali zote, ni lazima tuhakikishe kwamba uaminifu unadumishwa,” amesema mwanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo, EU inaeleza kuwa inachunguza chaguzi nyingine na mamlaka ya Kongo, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kudumisha ujumbe unaojumuisha kundi dogo tu la wataalam wa uchaguzi ambao watafuatilia mchakato wa uchaguzi kutoka mji mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.