Pata taarifa kuu

Kapteni Traoré ampokea Waziri Mkuu wa zamani wa Côte d'Ivoire Guillaume Soro

Waziri Mkuu wa zamani wa Côte d'Ivoire Guillaume Soro amekutana Jumanne huko Ouagadougou na rais wa mpito wa Burkina Faso ambaye aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya 2022, Kapteni Ibrahim Traoré, rais wa Burkina Faso ametangaza katika taarifa.

Guillaume Soro, huko Paris Septemba 17, 2020.
Guillaume Soro, huko Paris Septemba 17, 2020. STEPHANE DE SAKUTIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu na Kapteni Traoré ulifanyika siku nane baada ya kiongozi huyo wa upinzani wa Côte d'Ivoire kukutana kwa mazungumzo na mkuu wa utawala wa kijeshi wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, ambaye pia aliingia madarakani kupitia mapinduzi mwezi Julai. Mwishoni mwa mkutano wake na Kapteni Traoré, Bw. Soro, aliyenukuliwa na ikulu ya rais wa Burkina Faso, ametangaza "kufurahishwa na mtazamo wake mkubwa wa masuala ya kikanda".

Ameipongeza Burkina Faso na viongozi wake kwa mapambano makali na muhimu dhidi ya ugaidi katika nchi yake. "Ninathibitisha kuunga mkono kikamilifu mapambano ya kishujaa ya watu wa Burkinabe Faso kurejesha usalama katika eneo lao," Bw. Soro ameandika kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

Tangu mwaka 2015, Burkina imekumbwa na ghasia zinazofanywa na makundi ya wanajihadi yenye mafungamano na Islamic State na Al-Qaeda ambayo tayari yalikuwa yakishambulia nchi jirani za Mali na Niger. Bw. Soro alirejea Afrika mapema mwezi wa Novemba baada ya zaidi ya miaka minne akiishi uhamishoni.

Guillaume Soro, kiongozi wa zamani wa waasi ambao ulidhibiti nusu ya kaskazini ya Côte d'Ivoire katika miaka ya 2000 na aliyekuwa Waziri Mkuu na spika wa Bunge la kitaifa, alikosana na Alassane Ouattara mnamo mwaka 2019, mwaka ambao alikimbilia uhamishoni. Alihukumiwa mwaka 2020 akiwa hayupo kifungo cha miaka 20 jela kwa "ubadhirifu wa fedha za umma" nchini Côte d4ivoire, kisha kifungo cha maisha mwaka mmoja baadaye kwa "kuhatarisha usalama wa taifa".

Nchini Burkina Faso, waranti ya kukamatwa ilitolewa mwaka wa 2016 na mahakama ya kijeshi dhidi yake kama sehemu ya uchunguzi wa jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mnamo mwaka 2015 baada ya kuanguka kwa utawala wa Rais Blaise Compaoré.Waranti hii ilifutwa kwa "njia za kidiplomasia".

Inashangaza sana kuona kwamba ninaweza kukanyaga tena ardhi ya Burkina Faso, shukrani kwa serikali ya kijeshi, ambapo serikali zinazodaiwa kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia zimekataa kutambua haki za raia kama mimi hapa, raia wa Afrika Magharibi kama mimi hapa,” amesema Bw. Soro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.