Pata taarifa kuu
SHERIA-SIASA

Senegal: Mahakama yabatilisha hukumu ya kumrejesha Sonko kwenye kinyang'anyiro cha urais

Uamuzi wa mahakama ya juu zaidi nchini Senegal ulikuwa unasubiriwa kwa hamu kujua iwapo mpinzani Ousmane Sonko anaweza kurejea kwenye kinyang'anyiro cha urais mwezi Februari mwaka ujao. Lakini Mahakama ya Juu imeamua vinginevyo. Imebatilisha uamuzi wa mahakama ulioamuru kusajiliwa upya kwa Ousmane Sonko kwenye orodha ya wapiga kura, ambayo ingelimruhusu kuwa mgombea na kuthibitisha kwamba kesi hiyo lazima isikilizwe upya.

Mwanamke akipita mbele ya Mahakama ya Juu zaidi mjini Dakar, Novemba 17, 2023. Mahakama ya Juu imebatilisha hukumu ambayo ingelimrejesha kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko katika kinyang'anyiro cha urais mwezi Februari 2024, ikibainisha kuwa kesi hiyo itasikilizwa tena.
Mwanamke akipita mbele ya Mahakama ya Juu zaidi mjini Dakar, Novemba 17, 2023. Mahakama ya Juu imebatilisha hukumu ambayo ingelimrejesha kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko katika kinyang'anyiro cha urais mwezi Februari 2024, ikibainisha kuwa kesi hiyo itasikilizwa tena. © JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Rais wa Mahakama ya Juu amebatilisha na kufuta uamuzi wa mahakama ya Ziguinchor wa Oktoba 12. Uamuzi ambao uliamuru kusajiliwa upya kwa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko kwenye orodha za wapiga kura na hivyo kumruhusu kuwa mgombea urais.

Kwa mujibu wa jaji wa Mahakama ya Juu, mahakama ya Ziguinchor ilitafsiri vingine kasoro ya utaratibu; mpinzani alijulishwa kwa usahihi juu ya uamuzi wa kufutwa kwenye orodha ya wapiga kura, kulingana na mahakama hiyo hakukuwa sababu ya kumfuta.

Lakini Mahakama ya Juu pia imerudisha kesi hiyo katika mahakama ya Dakar kwa ajili ya kusikilizwa upya kuhusu undani wa kesi hiyo.

Kwa upande wa wafuasi wa Ousmane Sonko ni masikitiko makubwa. Hasa kwa vile mwendesha mashtaka wa umma alikuwa amemtaka jaji wa Mahakama ya Juu kuthibitisha kusajiliwa upya kwa Ousmane Sonko kwenye orodha za wapiga kura.

Hatimaye, kutokuwepo kwa mmoja wa majaji 5 wakati uamuzi huo ukisomwa kulitafsiriwa kuwa kuna uwezekano wa kukataliwa na watu waliofika kusikiliza uamuzi wa mahakama ya Juu.

Kwa sababu Hata kama kimsingi kila kitu bado kinawezekana na jaribio hili jipya, kwa kweli, miezi mitatu na nusu kabla ya uchaguzi wa rais, ni hali ambayo inaonekana kuwa haitawezekana kushinda kesi hii. Kwa sababu hakuna tarehe ya mahakama ya Dakar kujibu tena kesi hiyo ambao imetangazwa.

Serikali inacheza mchezo wa paka na panya, amebainisha mmoja wa mawakili wa Ousmane Sonko ambaye amesema anasikitishwa sana na uamuzi huu, na hivyo kuwanyima Wasenegali uchaguzi ambao mtu maarufu zaidi wa upinzani angeweza kushiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.