Pata taarifa kuu

Sudan: Jeshi linawazuia watoto waliokuwa wanatumikishwa kama wapiganaji na RSF

Nairob – Jeshi la Sudan linasema limewazuia watoto waliokuwa wamelazimishwa kuwasaidia wapiganaji wa kundi la RSF katika makabiliano yanayoendelea.

Mapigano yamekuwa yakiendelea kati ya wapiganaji wa RSF na jeshi la serikali ya Sudan kwa miezi kadhaa sasa licha ya wito wa kimataifa wa kutaka kusitishwa kwa vita
Mapigano yamekuwa yakiendelea kati ya wapiganaji wa RSF na jeshi la serikali ya Sudan kwa miezi kadhaa sasa licha ya wito wa kimataifa wa kutaka kusitishwa kwa vita AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa televisheni inayomilikiwa na serikali ya Sudan, watoto hao ambao idadi yao haijawekwa wazi, walikuwa waanzuiliwa katika eneo la Wadi Saidna, kaskazini mwa mji wa Khartoum.

Tarehe 15 ya mwezi Septemba, jeshi la Sudan liliwasilisha watoto 30 waliokuwa wanazuiliwa kama wafungwa wa kivita kwa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu.

Wapiganaji wa RSF wamekuwa wakituhumiwa mara kwa mara kwa kujihusisha na visa vya ukiukaji wa sheria za kimataifa kwa kuwasajili watoto katika mzozo unaoendelea nchini Sudan.

Mapigano yamekuwa yakiendelea kati ya wapiganaji wa RSF na jeshi mjini Khartoum, Darfur na Kordofan licha ya wito wa kusitishwa kwa vita hivyo ambavyo vimewaathiri maelfu ya watu.

Wito umendelea kutolewa kwa kurejelewa kwa mazungumzo ya nchini Saudi Arabia yanayolenga kuafikia makubaliano ya kumaliza mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.