Pata taarifa kuu

Kenya kutuma ujumbe wa kwanza Haiti kabla ya kuwapeleka polisi

Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Kithure Kindiki, amesema kuwa nchi hiyo itatuma wajumbe wa kutathmini hali nchini Haiti kabla ya kutumwa kwa maafisa wa polisi kupambana ghasia za magenge yanayowahangaisha raia.

Mnamo Agosti, Kenya ilituma ujumbe wake wa kwanza kuangazia hali halisi nchini Haiti
Mnamo Agosti, Kenya ilituma ujumbe wake wa kwanza kuangazia hali halisi nchini Haiti © Brian Inganga / AP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Agosti, Kenya ilituma ujumbe wake wa kwanza kuangazia hali halisi nchini Haiti.

Aidha waziri Kindiki amesema kuwa maafisa hao wana vifaa vya kukabiliana na magenge yenye silaha nchini Haiti kutokana na namna wamefanya kazi kwa mafanikio katika nchi kadhaa walikotumwa hapo awali, ikiwemo Namibia, Kambodia, iliyokuwa Yugoslavia, Bosnia na Herzegovina, Croatia na Sierra Leone.

Maofisa wa polisi wa kenya wanatarajiwa kwenda kuwasaidia wenzao wa Haiti kuyakabili magenge ya kihalifu
Maofisa wa polisi wa kenya wanatarajiwa kwenda kuwasaidia wenzao wa Haiti kuyakabili magenge ya kihalifu REUTERS - RALPH TEDY EROL

Aliongeza kuwa maafisa wa polisi ni sehemu ya vikosi vya usalama vya Kenya vilivyotumwa hivi sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Somalia na Sudan Kusini kurejesha hali ya utulivu.

Hata hivyo, amesema kuwa hatua hiyo ya kuwatuma polisi kwenye taifa la Haiti, itafanyika baada ya kuafikia vigezo vyote vya kisheria, ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na bunge la kitaifa na lile la seneti.

Magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yakitatiza usalama wa raia wa Haiti
Magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yakitatiza usalama wa raia wa Haiti AP - Odelyn Joseph

Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa uliidhinisha kutumwa kwa maafisa wa polisi wa Kenya nchini Haiti lakini mahakama siku ya Jumatatu ilisimamisha kwa muda mpango huo kusuburi kuamuliwa kwa kesi iliyowasilishwa kufahamu iwapo hatua hiyo ni kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.