Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Togo: Kutokuwepo kwa kalenda ya uchaguzi kunatia wasiwasi upinzani

Nchini Togo, bunge litamaliza muhula wake ndani ya kipindi cha miezi mitatu, lakini bado hakuna tarehe iliyopangwa kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge na wa magavana, ambao ulipaswa kuandaliwa mwishoni mwa mwaka huu. Upinzani una wasiwasi na unaomba mijadala ili kuandaa kipindi cha mpito.

Zoezi la uhesabu kura katika kituo cha kupigia kura huko Lomé, Jumamosi Februari 22, 2020.
Zoezi la uhesabu kura katika kituo cha kupigia kura huko Lomé, Jumamosi Februari 22, 2020. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Kutokuwepo kwa kalenda ya uchaguzi kunatia wasiwasi upinzani wa Togo, muungano wa upinzani umebaini. "Mwishoni mwa mwezi Novemba, chaguzi hizi lazima zifanyike", amesema Brigitte Adjamagbo-Johnson, mratibu wa muungano w upinzani. Muungano wa vyama vya upinzani ulilaani sensa ya wapiga kura ambayo haikukamilika mwezi Juni mwaka mwaka huu. Leo, muungano huo unatoa wito kwa upana zaidi kwa "majadiliano madhubuti juu ya masharti ya kipindi cha mpito nchini Togo".

Ndani ya serikali ya Togo, wanabaini kwamba mfumo wa kudumu wa mazungumzo haya upo, lakini upinzani haujatoa rasmi malalamiko yake. Chanzo hicho cha serikali kinatambua kuwa itakuwa vigumu kuandaa uchaguzi ifikapo mwisho wa mwaka nchini Togo, lakini kwamba kucheleweshwa kwa mwezi mmoja au wiki sita kunawezekana.

Kuhusu chama cha wengi cha UNIR, kiongozi wake hana wasiwasi: nakala zetu zinatoa muendelezo wa mamlaka katika Bunge la kitaifa la Togo, amesema Acholi Aklesso. Kuna umuhimu gani wa kuweka ratiba, ikiwa Tume ya Uchaguzi (CENI) haiko tayari, amebainisha. Hata hivyo CENI tumejarbu kuitafuta lakini haikutaka kujibu maswali yetu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.