Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

DRC: Floribert Anzuluni ateuliwa kupeperusha bendera ya mashirika ya kiraia

Mashirika ya kiraia, makundi mbalimbali ya kiraia, vyama vya kisiasa pamoja na watu binafsi, wanachama wa Alternative for A New Congo (ACN), wamemteua mgombea wao kwa uchaguzi wa urais wa mwezi Disemba 2023. Mwanaharakati Floribert Anzuluni ameibuka kuwa chaguo la pamoja dhidi ya mwandishi wa habari wa zamani Joelle Bilé baada ya duru ya pili ya kura ya mchujo iliyofanyika Alhamisi, Oktoba 5, mjini Kinshasa.

Moja ya maeneo ya mji wa Kinshasa, mji mkuu wa DRC. Uchaguzi wa mchujo wa vyama vya kiraia ulifanyika siku ya Alhamisi Oktoba 5.
Moja ya maeneo ya mji wa Kinshasa, mji mkuu wa DRC. Uchaguzi wa mchujo wa vyama vya kiraia ulifanyika siku ya Alhamisi Oktoba 5. © Wikimedia commons / CC BY-SA 4.0
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi

Mtoto wa aliyekuwa rais wa Bunge, Floribert Anzuluni alikulia katika mazingira ya kisiasa. Lakini kwa yote hayo, alijijengea jina ndani ya mashirika ya kiraia kwa kuanzisha vuguvugu la kiraia la Filimbi, ambalo lilionekana kuwa na nguvu wakati wa mapambano kwa minajili ya mabadiliko ya kisiasa kabla ya kuwasili kwa Félix Tshisekedi madarakani.

Uanaharakati wake ulimlazim kukimbilia uhamishoni mwaka wa 2015, huku baadhi ya wenzake wakijikuta gerezani. Mfanyabiashara huyu mwenye umri wa miaka 40 pia alichukua jukumu kubwa katika vita dhidi ya ufisadi ndani ya shirika la Marekani la The Sentry.

Kura za mchujo katika mashirika ya kiraia

Kwa hivyo, chaguo la Floribert Anzuluni ni matokeo ya kura za mchujo ndani ya mashirika ya kiraia, ambayo yanamtofautisha na wagombea wengine wa urais. Waanzilishi wa chaguzi hizi za mchujo wanasema wanataka kupindua dhana ya kisiasa iliyotawala nchini DRC, inayojulikana kulingana nao na mamlaka ya kimaadili ambayo hufanya maamuzi ya upande mmoja na kuweka matakwa yake kwa kila mtu.

Wakati duru ya pili ya kura za mchujo ikiendelea, wagombea wengine wawili walisajiliwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI). Marie-José Ifoku, ambaye alikuwa mgombea mwanamke pekee mwaka wa 2018, anagombea tena. Hatimaye, Georges Buse Falay, mkurugenzi wa zamani katika ofisi ya rais wa zamani Laurent-Désiré Kabila, anagombea kama mtu binafsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.