Pata taarifa kuu
WIZI WA MAGARI

Usafirishaji wa magari kwenda Afrika: Mashitaka saba yafunguliwa Paris

Kontena lililokuwa limebeba magari yaliyokuwa yakielekea Afrika Magharibi lilinaswa siku ya Jumanne nchini Uhispania, kama sehemu ya uchunguzi kuhusu mtandao ambao tayari umesababisha mashtaka saba nchini Ufaransa, chanzo cha polisi kimesema siku ya Jumanne.

Kulingana na Ofisi Kuu inayopambana dhidi ya Uhalifu uliopangwa, Ufaransa ni "moja ya nchi za Ulaya kunakoripotiwa wizi mwingi wa magari".
Kulingana na Ofisi Kuu inayopambana dhidi ya Uhalifu uliopangwa, Ufaransa ni "moja ya nchi za Ulaya kunakoripotiwa wizi mwingi wa magari". © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kukamatwa kwa kontena nyingine, katika mji wa bandari wa Algeciras nchini Uhispania, kunafuatia matukio mawili ya kukamatwa kwa kontena huko Le Havre (kaskazini-magharibi) na moja huko Las Palmas (Uhispania), chanzo hiki kimeliambia shirika la habari la AFP, wakati uchunguzi ukiendelea. Mnamo Septemba 12, tukio la kwanza la kukamatwa kwa kontena lililenga "katika mazingira magumu" mtandao huu "unaoendesha harakati zake", Guillaume Maniglier, naibu mkuu wa Ofisi Kuu ya Mapambano dhidi ya Uhalifu uliopangwa (OCLCO), ameelezea AFP.

Kukamatwa huku kulisababisha kufunguliwa mashitaka mnamo Septemba 15 ya wanaume saba, watatu kati yao waliwekwa kizuizini kabla ya kesi, kwa wizi wa genge lililoandaliwa na kupokea bidhaa zilizoibiwa na genge lililoandaliwa, kulingana na chanzo cha mahakama. "Magari 180 yalipitia mikononi mwa kundi hili" na "kontena kadhaa zilitumwa kwa kila wiki," amesema Bw. Maniglier.

Wachunguzi themanini kutoka OCLO, polisi, wakiungwa mkono na timu kadhaa na wachambuzi kutoka Europol na Interpol waliweza kuzuia "dazeni kadhaa" za magari yaliyokuwa yakiondoka, lakini "mengine yalikuwa tayari yamefikishwa Afrika Magharibi" .

Kulingana na Bw. Maniglier, Ufaransa ni "moja ya nchi za Ulaya kunakoripotiwa wizi mwingi wa magari": "Mnamo 2021, magari 121,000 yaliibwa, na mnamo 2022, magari 135,000 yaliibwa". Uchunguzi huu, uliozinduliwa katika msimu wa joto wa mwaka 2021 chini ya uangalizi wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Paris, ulitaja haraka uhusiano "na Uswisi, Ujerumani, Uhispania, Ubelgiji, ambapo magari yalitumwa kuhifadhiwa".

Mmoja wa wanaodaiwa kuwa wafadhili, raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 38 huko Essonne, alihalalisha safari zake kati ya Ufaransa, Ubelgiji na Uswisi kwa nia yake ya kuomba hifadhi katika nchi hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.