Pata taarifa kuu

Somalia: Serikali yaitaka Atmis kusitisha zoezi la kuondoa vikosi vyake

Serikali ya Somalia inaiomba Atmis, Ujumbe wa Mpito wa Umoja wa Afrika, kusitisha operesheni ya kuondoa vikosi vyake nchini humo. Mshauri wa usalama wa rais, Hussein Sheikh Ali, alitoa ombi hilo siku ya Jumanne katika barua iliyotumwa kwa balozi wa Umoja wa Mataifa, Ferit Hoxha. Anaomba "usitisho wa kiufundi" ili kuwapa wanajeshi wa Somalia muda wa kuunganisha ushindi wao dhidi ya magaidi wa Al Shabab.

Mwanajeshi wa Somalia katika kambi ya kijeshi ya Sanguuni, mwaka wa 2018.
Mwanajeshi wa Somalia katika kambi ya kijeshi ya Sanguuni, mwaka wa 2018. AFP - MOHAMED ABDIWAHAB
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa odisi ya rais wa Somalia, bado ni mapema mno kuona wanajeshi wa Atmis wakiondoka. Ana wasiwasi sana kuhusu usalama wa ya wakimbizi walio karibu na vituo vya jeshi vya Umoja wa Afrika. Serikali ya Somalia inataka "mpango wa kina" kwa ajili ya ulinzi wao, hasa kwa vile awamu ya 2 ya operesheni ya kujiondoa kwa vikosi vya Atmis inahusu kambi zilizotengwa.

Atmis ilianza kujiondoa mwanzoni mwa mwaka, ili kuruhusu vikosi vya Somalia kuchukua nafasi. Mamlaka wanatambua kwamba jeshi la taifa bado halina uwezo wa kudhibiti eneo lake. "Mnamo Agosti 26, tulipatwa na matatizo kadhaa […] na vikosi vyetu vililazimika kuondoka katika miji iliyokombolewa hivi majuzi," imeandikwa kwenye barua hiyo. Siku ya Jumatatu, Atmis ilizindua awamu ya 2 ya operesheni yake ya kuondoka nchini Somalia.

Wakiacha funguo za kambi ya Biyo Adde, karibu na Mogadishu, kamanda wake, Luteni Kanali Philippe Butoyu hata hivyo alitangaza kwamba "vikosi vya usalama vya Somalia vimeonyesha uwezo wao unaokua wa kulinda nchi. » Awamu ya 2 ya operesheni ya kuondoka Somalia kwa vikosi vya Atmis inatoa nafasi ya kuondoka kwa wanajeshi 3,000 kufikia mwisho wa mwaka huu. Wanajeshi 14,000 watakaosalia wataondoka Somalia kufikia mwisho wa mwaka 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.