Pata taarifa kuu

Mali: Wapiganaji wa CSP wajiondoa katika mji wa Léré

Nchini Mali, wapiganaji wa Mfumo wa Kimkakati wa Kudumu (CSP) wamejiondoa katika mji wa Léré. Muungano huu wa makundi yenye silaha kutoka Kaskazini ulishambulia na kuchukua udhibiti wa kambi ya kijeshi ya Mali katika mji huo huko Niafunké, katika jimbo la Timbuktu Jumapili Septemba 17 mchana. Makao makuu ya Jeshi la Mali (FAMA) yanathibitisha shambulio hilo na kupendekeza jibu stahiki. Lakini washambuliaji waliondoka mjini wakati wa usiku.

Askari wa Mali wanaingia katika helikopta ya Jeshi la Ndege la Mali huko Léré, katikati ya nchi hiyo
Askari wa Mali wanaingia katika helikopta ya Jeshi la Ndege la Mali huko Léré, katikati ya nchi hiyo Anthony Fouchard/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huo Bamako, David Bache

Nchini Mali, wapiganaji kutoka Mfumo wa Kimkakati wa Kudumu (CSP) walijiondoa kabisa kutoka Léré kati ya saa nane na saa tisa usiku wa leo. Hivi ndivyo mmoja wa wasemaji wao anavyobainisha, ambaye anasema kuwa kujiondoa huku kunanuiwa kuepusha mashambulizi yanayoweza kufanywa na jeshi la Mali. Kujiondoa kwa wapiganaji wa CSP katika mji wa Léré kunathibitishwa na vyanzo kadhaa vya kiraia. Hali ya utulivu inatawala mjini kwa sasa.

Hakuna ripoti iliyotumwa na CSP, wala na jeshi la Mali ambalo lilitoa taarifa jana jioni na leo Jumatatu Septemba 18 asubuhi, kushutumu "mashambulizi ya vikosi vya uovu dhidi ya kambi ya kijeshi ya Léré", na kuhakikisha kuwa vimehamasishwa "kutetea ngome zake. ” na “kudumisha usalama wa raia”

Jumapili alasiri, CSP ilivamia mji wa Léré na kuchukua udhibiti wa kambi ya kijeshi ya mji huo "baada ya masaa mawili ya mapigano", kulingana na makundi ya waasi wenye silaha, ambao pia wanadai kuidungua ndege ya jeshi la Mali, na kutoa ushahidi. Vyanzo vya raia na usalama katika eneo hilo vimethibitisha kuwa CSP imeteka kambi ya kijeshi ya Mali. Kabla, ya kujiondoa.

Mnamo Septemba 12, kami ya wanajeshi wa Mali (FAMA) huko Bourem, katika jimbo la Gao, ililengwa na CSP. Tayari waasi hao walikuwa wameshafanya mashambulizi ya haraka kabla ya kuondoka. Kambi zote mbili zilikuwa zimetaja vifo vingi, lakini hakuna ripoti sahihi ya kuaminika na huru ambayo inaweza kupatikana. CSP baadaye ilitoa video ya mwanajeshi wa Mali, aliyekamatwa wakati wa shambulio hili na tangu wakati huo anashikiliwa mfungwa.

CSP inazingatia kwamba operesheni zake za hivi majuzi zinajumuisha "kujilinda" na inalishutumu jeshi la Mali na washirika wake wa Urusi kutoka kundi la Wagner kwa kukiuka makubaliano ya amani ya 2015 mara nyingi katika miezi ya hivi karibuni na usitishaji mapigano uliokuwa ukitekelezwa.

Mamlaka ya mpito ya Mali imeendelea kulaani "mashambulizi ya kigaidi" katika wiki za hivi karibuni. Jumamosi Septemba 16, waliunda na nchi jirani za Niger na Burkina Faso, "Muungano wa Mataifa ya Sahel", ambayo hutoa ushirikiano mpana kukabiliana na hatari ya ugaidi lakini pia "shambulio lolote dhidi ya uhuru na uadilifu wa eneo" la nchi hizi tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.