Libya:Kimbunga Daniel chaua watu zaidi ya 2,000
Nairobi – Takriban watu 2,000 wafariki katika mafuriko yaliyotokea mashariki mwa Libya kutokana na dhoruba ya kimbunga Daniel ambacho kimepiga katika bahari ya Mediterania.
Imechapishwa:
Taarifa hiyo ya vifo vya watu 2,000 imetolewa na Waziri Mkuu wa serikali ya Mashariki mwa Libya Ossama Hamad alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha al-Masar. Vilevile Hamad amasema kuwa kuna idadi kubwa ya raia hawajulikani waliko.
Picha zilizochukuliwa na wakazi wa eneo la maafa, zimeonyesha maporomoko makubwa ya matope, majengo yaliyoanguka na vitongoji vyote vilivyozama chini ya maji.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa, picha zilizoonekana kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakiwa wamekwama juu ya magari yao wakati wakijaribu kupata msaada katika mafuriko hayo makubwa, wakati kimbunga Daniel kikipiga miji ya Benghazi, Sousse, Al Bayda, Al-Marj na Derna.
Vikosi vya uokoaji vimepelekwa kwenye mji huo, ulioko takriban kilometa 900 mashariki mwa mji mkuu, Tripoli wakatiu huu Mamlaka zilkitangaza hali ya mbaya ya hatari, na kufunga shule na maduka pamoja na kuweka amri ya kutotoka nje.
Tayari serikali ya Mashariki imetangaza siku tatu za maombolezo kufuatia mkasa huo, Tawfik al Shukri ni msemaji wa shirika la msaada la Red Crescent.
Wafanyakzi wote wamekuwepo kila mahali tangu kutokea kwa mkasa, Jijini Darna, kwa mujibu wa serikali. Kuna zaidi ya miili 2,030 iliyopatikana na zaidi ya watu 9,800 hawajulikani walipo.Kuna vijiji 5 huko Darna ambavyo vimeharibiwa kabisa na maji. Hali ni mbaya sana ... baada ya masaa ya kwanza ya mafuriko, mabwawa yalitolewa. Shirika la hili tayari limepoteza wanachama watatu wakati wa oparesheni ya uokoaji. Lazima tuunganishe juhudi za zetu : serikali mbili za Libya, masharika ya ndani na ya kimataifa ili tuweze kuwasaidia watu kwa uwepesi. Amesema Tawfik al Shukri.
TAWFIK AL SHUKRI MSEMAJI WA SHIRIKA LA MSAADA LA RED CRESCENT Red