Pata taarifa kuu

Wanajeshi watatu wafungwa kwa 'njama dhidi ya usalama wa serikali' nchini Burkina

Wanajeshi watatu wa Burkina Faso wanaotuhumiwa kutaka "kuvuruga" utawala wa kijeshi uliotokana na mapinduzi ya kijeshi, wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya "njama dhidi ya usalama wa taifa", mwendesha mashtaka wa kijeshi wa Ouagadougou ametangaza siku ya Ijumaa.

Moja ya maeneo muhimu, katika mji wa Ouagadougou.
Moja ya maeneo muhimu, katika mji wa Ouagadougou. © Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa kijeshi ilifikishiwa malalamiko kuhusiana na kukamatwa mwezi Agosti "kwa askari na askari wa zamani, kupitia taarifa za kijasusi, kuhusiaa na njama dhidi ya usalama wa taifa kwa kulenga nyumba kadhaa ikiwa ni pamoja na ile ya rais wa mpito - Ibrahim Traoré - na zile za baadhi yaviongozi wa kiraia na kijeshi kwa nia ya kuvuruga serikali ya mpito".

Kufuatia shutuma hizo, uchunguzi wa kina ulifunguliwa na "hadi sasa, askari watatu wanaohusika wamekamatwa na kufikishwa kwa jaji anayechunguza kesi hiyo na kuwaweka katikakizuizini kwa vitendo vya njama za kijeshi, ukiukaji wa amri za kijeshi, njama " dhidi ya usalama wa taifa, ushirikiano na kundi la wahalifu na kuhatarisha maisha ya wengine," Kamanda Alphonse Zorma, mwendesha mashtaka wa kijeshi, amesema.

Wanajeshi hao watatu ni Windinmalégdé Kaboré, Brice Ismaël Ramdé na askari wa zamani Sami Dah, aliyefutwa kazi kwa sababu alipatikana na hatia katika kesi nyingine ya kula njama dhidi ya serikali mwaka wa 2015.

"Wamekiri makosa," amesema Bw. Zorma.

Mnamo mwezi wa Desemba, ofisi ya mashtaka ya kijeshi ilishutumu jaribio lingine la "kuvuruga taasisi za serikali" likihusisha hasa raia na afisa mkuu, Luteni Kanali Emmanuel Zoungrana, ambaye tayari amefungwa kwa vitendo kama hivyo.

Kapteni Traoré alimpindua Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba mnamo Septemba 2022, aliyeongoza mapinduzi mnamo Januari 2022 dhidi ya rais mteule Roch Marc Christian Kaboré, anayeshutumiwa kwa kutoweza kupigana dhidi ya ghasia za wanajihadi ambazo zimeikumba nchi hiyo tangu 2015.

Mashambulizi haya yanayohusishwa na makundi yenye mafungamano na Al-Qaeda na Islamic State yamesababisha vifo vya watu 16,000 na wengine milioni mbili kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.