Pata taarifa kuu
USALAMA-MAANDAMANO

Goma: Watu 7 wauawa katika makabiliano kati ya polisi na kundi la Wazalendo

Watu saba waliuawa na wengine karibu ishirini kujeruhiwa katika makabiliano yaliyotokea Jumatano Agosti 30 huko Goma (Kivu Kaskazini), kati ya polisi na kundi la wafuasi wa kanisa la Wazalendo.

Kulingana na vyanzo vya ndani, makabiliano haya yalitokea katika wilaya za Magharibi na Kaskazini za mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma.
Kulingana na vyanzo vya ndani, makabiliano haya yalitokea katika wilaya za Magharibi na Kaskazini za mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma. AFP - CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vya ndani, mapigano haya yalitokea katika wilaya za Magharibi na Kaskazini za mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma, klingana na Radio OKAPI.

Kwa mpango wa kanisa la Wazalendo, maandamano haya, yaliyopigwa marufuku na mamlaka ya kisiasa, yaliandaliwa dhidi ya MONUSCO pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Vyanzo hivyo vinaripoti kwamba milio ya risasi ilisikika mwendo wa saa tisa na dikaka 45 usiku katika vitongoji vya Kyeshero, Ndosho, Himbi, Katoyi na Kasika.

Katika wilaya ya Kyeshero, kwa mfano, kituo cha Redio na televisheni, Uwezo wa neno, kinachojulikana kwa jina la Wazalendo redio ya mchungaji Efraim Bisimwa, kililengwa zaidi na makabiliano hayo.

Waumini 6 wa kanisa la Wazalendo walioeneza jumbe za mwito huu wa maandamano waliuawa pao hapo.

Miongoni mwao ni mwanamke, mshirika wa karibu na Mchungaji Ephraim Bisimwa.

Baadhi ya vyanzo vya habari vinaeleza kuwa mchungaji huyu alikamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya jiji hilo.

Mapigano mengine yaliripotiwa katika vitongoji vingine kadhaa ambapo uharibifu ulirekodiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.