Pata taarifa kuu

Somalia: Al-Shabab wamedai kuteka maeneo mawili yaliyokuwa yamechukuliwa na jeshi

Wapiganaji wa al-Shabab wanaohusishwa na kundi Islamic State wamedai kuteka tena maeneo mawili yaliokuwa yamechukuliwa na jeshi la Somalia wakati wa vita dhidi ya kundi hilo.

Al Shabaab imewauawa makumi kwa maelfu ya watu tangu mwaka wa 2006 nchini Somalia
Al Shabaab imewauawa makumi kwa maelfu ya watu tangu mwaka wa 2006 nchini Somalia REUTERS/Feisal Omar/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinaeleza kuwa pande zote mbili zimeripoti hasara kubwa wakati wa makabiliano ya kuchukua udhibiti wa mji wa Cowsweyne.

Vyanzo vya karibu na hosipitali ya kijeshi nchini humo vimesema karibia wanajeshi 50 waliokuwa wamejeruhiwa waliletwa kwenye hosipitali hiyo kwa matibabu.

Haya yanajiri wakati huu rais Hassan Sheikh Mohamud akiwa ameapa kumaliza kundi hilo katika kipindi cha miezi michache.

Siku ya Ijumaa jeshi na wanamgambo wanaounga mkono serikali walisherehekea kutekwa kwa ngome ya al-Shabab, El Bur.

Hata hivyo kutekwa tena kwa kijiji cha karibu cha Wabho kunaonyesha kuwa wanajeshi wako katika hatari ya kushambuliwa katika maeneo ambayo wanajihadi wamejikita kwa muda mrefu.

Al Shabaab imewauawa makumi kwa maelfu ya watu tangu mwaka wa 2006 katika kile kinachotajwa ni juhudi za kundi hilo kuangusha serikali ya Somalia inayooungwa mkono na Magharibi .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.