Pata taarifa kuu

Mali: Minusma yaendelea kuwaondoa wanajeshi wake nchini Mali

Zaidi ya miezi mitatu baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali la kuomba "ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali kuondoa wanajeshi wake nchini humo, zoezi hilo linaendelea. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa tayari umeondoa wanajshi wake katika kambi tatu kati ya kumi na mbili ilizokuwa ikishikilia, ile ya Ogossagou katika jimb la kati, na zile za Ber na Goundam katika jimbo la Timbuktu. Kulingana na chanzo cha Umoja wa Mataifa, zoezi la kuwaondoa wanajeshi wa MINUSMA linaendelea.

Walinda amani wa MINUSMA huko Kidal.
Walinda amani wa MINUSMA huko Kidal. REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Kambi ya Ménaka kaskazini mashariki mwa Mali itafungwa hivi karibuni, ni kambi ya nne ambayo MINUSMA inaondoa wanajeshi wake. Lengo linalofuata lililowekwa na ujumbe huu ni kuwaondoa wanajeshi wake katika kambi za Grand Nord: itafuatiwa na kufungwa kwa msingi ya Kidal na kambi za Mopti na Ansongo.

Kuanzia tarehe 31 Desemba 2023, hakutakuwa na wanajeshi tena kutoka MINUSMA nchini Mali. "Ratiba itaheshimiwa" kilihakikishia chanzo cha Umoja wa Mataifa: azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliweka tarehe hii yiwe muda wa mwisho wa kuondolewa kabisa kwa wanajeshi wa MINUSMA nchini Mali.

Baada ya muda huu, hata hivyo, vifaa bado vitalazimika kuhamishwa kutoka kambi za Gao, Bamako na pengine huko Timbuktu. Hatua hii itaanza Januari 1 na ufunguzi wa awamu ya "kukabidhi" rasmi kambi hizo, kulingana na azimio hilo.

Baada ya miaka kumi ya operesheni nchini Mali, changamoto za vifaa ni kubwa, kinabainisha chanzo chetu cha Umoja wa Mataifa. Kwa upande wa kijeshi pekee, ujumbe huo lazima uondoe makontena 5,000 ya vifaa ili kurejeshwa kwa nchi ambazo zilichangia kwa wanajeshi.

Kando na zana za kijeshi, sehemu ya rasilimali za ujumbe huo zinaweza kuhamishiwa kwenye misheni nyingine za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.