Pata taarifa kuu

Ethiopia: Baada ya miaka miwili ya vita, Ashenda yasherehekea tena mjini Addis Ababa

Wakilengwa kwa sababu ya asili yao wakati wa miaka miwili ya mzozo wa kikatili kati ya serikali ya shirikisho na mamlaka ya eneo la Tigray, wakaazi wa jimbo hilo kwa mara nyingine tena watasherehekea Ashenda, tamasha la jadi la wanawake kaskazini mwa Ethiopia.

Mwaka mmoja kabla ya mzozo huo kuzuka ambao ulikumba Ethiopia katika eneo la kaskazini kati ya mwezi Novemba 2020 na Novemba 2022, UVIKO-19 ilizuia sherehe za Ashenda.
Mwaka mmoja kabla ya mzozo huo kuzuka ambao ulikumba Ethiopia katika eneo la kaskazini kati ya mwezi Novemba 2020 na Novemba 2022, UVIKO-19 ilizuia sherehe za Ashenda. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Hatujasherehekea Ashenda kwa muda mrefu" kwa sababu ya vita katika jimbo la Tigray na kurejea kwa amani "kunafanya tamasha hili kusherehewa tena", anaelezea Danawit Tesfaye, ambaye atasherehekea sikukuu hii ya kitamaduni ya wanawake huko Addis Ababa kwa sikuu hii ya kijadi ya wanawake wa kaskazini mwa Ethiopia.

Pia ni fursa kwa wale ambao, kama mwanadada huyu mwenye umri wa miaka 23, waliojaa mbele ya Ukumbi wa Milenia ambapo sherehe zinafanyika, kuonyesha mchana kweupe, kupitia nguo zao na staili zao, utambulisho wao wa Tigray, baada ya tamasha kutoadhimishwa kwa miaka miwili ya mzozo wa kikatili kati ya serikali ya shirikisho na mamlaka ya jimbo la Tigray.

Mbali na mzozo huu, takriban miongo mitatu (1991-2017) ya utawala wa kimabavu wa kisiasa wa wachache wa wakaazi wa Tigray (5% ya wakazi)kwenye mamlaka ya shirikisho ya Ethiopia, imeibua chuki miongoni mwa baadhi ya makabila 80 ya Ethiopia.

Mtaani, kundi dogo watu wanacheza kwa fahari wakishikilia bendera ya jimbo la Tigray. Tukio lisiloweza kufikiria hadi hivi majuzi katika mji mkuu, ambapo Watigraya walikuwa, wakati wa vita na kama mahali pengine nchini Ethiopia, walengwa wa kamata kamata kwa misingi ya kikabila.

Ashenda tamasha la kijadi lenye asili ya Tigray, pia inaadhimishwa katika jimbo jirani la Amhara na Eritrea, jimbo la zamani la Ethiopia linalopakana na Tigray. Hapo awali, tamasha la kidini la kuadhimisha mwisho wa Filseta, mfungo wa siku 15 unaohusisha kila upande wa Asumption, Ashenda imebadilika na kuwa sherehe zinazovuka dini na kuashiria uhuru wa wanawake na wasichana.

Mwaka mmoja kabla ya mzozo huo kuzuka ambao ulikumba Ethiopia kaskazini kati ya mwezi Novemba 2020 na Novemba 2022, na kuangaziwa na dhuluma mbaya ikiwa ni pamoja na ubakaji mwingi, UVIKO-19 ilizuia sherehe hizo.

"Hatujasherehekea" Ashenda "kwa miaka mitatu iliyopita kwa sababu watu wetu huko Tigray walikuwa (...) vitani", anaeleza Selam Haile, 15, karibu na jukwaa la Milenia ambapo wasanii wa Tigray watapishana ukumbini.

"Ilikuwa mbaya kwetu, kwa sababu (Ashenda) ni siku ya uhuru," anaongeza, "inamaanisha uhuru kwa wasichana, wasichana na watu wazima. Kusherehekea Ashenda baada ya miaka hii mitatu ni muhimu sana kwetu (...) wasichana wako huru wakati wa Ashenda, wanavaa, wanapamba mikono yao (na hina), hufanya mambo mengi".

Pembezoni na ndani ya chumba hicho, vijana, wanawake na wasichana wadogo wakisindikizwa na mama zao wanacheza ngoma, wakiwa wamevalia "habesha kemis" - nguo za kitamaduni za pamba mnene nyeupe zilizopambwa kwa taraza za rangi - au nguo za rangi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.