Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC yaandaa vikao kuhusu hali ya kuzingirwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri

Vikao kuhusu tathmini ya hali ya kuzingirwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri vinafunguliwa Jumatatu hii, Agosti 14 katika makao makuu ya Baraza la Wawakilishi mjini Kinshasa.

Makao makuu ya Baraza la Wawakilishi la DRC huko Kinshasa,
Makao makuu ya Baraza la Wawakilishi la DRC huko Kinshasa, © Wikimedia Commons CC-BY 2.0 Antoine Moens de Hase
Matangazo ya kibiashara

Hali ya kuzingirwa katika mikoa ya Kivu Kakazini na Ituri inatarajiwa kujadiliwa leo Jumatatu Agosti 14, 2023, majadiliano ambayo yataendelea hadi Jumatano Agosti 16.

Majadiliano ya Jedwali hili la pande zote yataleta pamoja:

Wajumbe wa Ofisi ya rais wa Jamhuri,

wa Baraza la Bunge,

wa Bunge la Seneti, wa Serikali,

wa mahakama,

mabunge ya majimbo,

serikali za mikoa

na viongozi wa kimila;

viongozi wa kidini, mashirika na vyama vinavyotambulika, Shirikisho la Biashara la Kongo pamoja na wataalamu.

Kwa mujibu wa msemaji wa Serikali, Patrick Muyaya, majadiliano ya Jedwali hili  yaliyopendekezwa na rais Félix Tshisekedi yanakuja baada ya vikao vilivofanyika kuanzia Jumatatu Juni 19 hadi Ijumaa Juni 23, ambavyo viliwezesha kutambua washiriki pamoja na mada zinazopaswa kushughulikiwa.

"Mapendekezo yatakayotolewa yatawasilishwa kwa Mkuu wa Nchi ili kuondoa mustakabali wa uamuzi huu", anabainisha Waziri Patrick Muyaya.

Suala la usalama ni kipaumbele katika majadiliano haya

Shirika moja la kiraia katika mji wa Goma linakaribisha kuitishwa kwa mkutano huu huku likitayarisha tathmini mseto ya utawala huu wa kipekee uliowekwa ili kuleta amani katika mikoa hii miwili.

Kiongozi wa shirika hili la kiraia, Marion Ngavo, anataka kuona washiriki katika vikao hivi wanaamua kwa usalama wa raia na sio kwa masilahi ya kisiasa.

"Kufanyika kwavikao hivi kuhusu hali ya kuzingirwa ni tukio linalosubiriwa kwa hamu na wakazi kuona jinsi ya kuamua juu ya usimamizi wa baadaye katika eneo la Mashariki mwa DRC, ili kuwa na amani, usalama na maendeleo. Hakika, katika kipindi cha hali ya kuzingirwa, kulikuwa na kupungua kwa migogoro ya kikabila katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Tumeshuhudia kuongezeka kwa mapato kutoka kwa watu masikini,” anamebaini Marion Ngavo.

Kurejesha amani

Kwa mujibu wa mbunge wa kitaifa Bertrin Mubozi akinukuliwa na Radio OKAPI, mwenyekiti wa Tume ya Ulinzi na Usalama katika Bunge la kitaifa, maamuzi yatakayochukuliwa wakati wa vikao hivi lazima yawahakikishie wakazi wa Mashariki juu ya kurejea kwa amani na usalama.

“Na hivyo tuelekeze mawazo yetu yote katika mwelekeo wa kujiaminisha kwamba katika ngazi ya utendaji kazi lakini pia katika ngazi ya menejimenti na utawala wa mikoa hii miwili, tunaweza kujipa moyo kwamba haya mawili yatashindana kwa lengo hili linalopendekezwa na rais wa Jamhuri na sisi sote: hatimaye kuona wakazi wa sehemu hii ya Jamhuri wanaishi kwa amani na usalama,” amependekeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.