Pata taarifa kuu

Vita nchini Sudan: Raia walazimika kutoroka makaazi yao kufuatia kuongezeka kwa ghasia Khartoum

Khartoum ilikumbwa na mapigano makali tarehe 7 na 8 Agosti 2023 asubuhi. mapigano makali ya silaha a makombora yalijikita zaidi katika maeneo ya Omdurman na Bahri. Mashambulio ya anga yalilenga vitongoji vilivyo na watu wengi. Jeshi la Sudan pia lilifanya mashambulizi ya anga ambayo yalilenga njia za ugavi za Rapid Support Forces (RSF), kundi la wanamgambo ambalo linakabiliana na jeshi la serikali tangu Aprili 15, 2023.

[Image d'illustration] Des obus sont vus sur le sol près des bâtiments endommagés du marché central lors d'affrontements entre les forces paramilitaires de soutien rapide et l'armée à Khartoum Nord, au Soudan.
[Image d'illustration] Des obus sont vus sur le sol près des bâtiments endommagés du marché central lors d'affrontements entre les forces paramilitaires de soutien rapide et l'armée à Khartoum Nord, au Soudan. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Wakati vita nchini Sudan vikiingia katika wiki yake ya kumi na tano, hali hii inawalazimu wakaazi wengine ambao walikuwa bado wamejificha majumbani mwao kuukimbia mji mkuu.

Ikiwa mapigano ya Khartoum yanawafanya raia kubaki majumbani mwao au kutoroka mji mkuu, katika wilaya ya Abu Rouf huko Omdurman, amri imetolewa ya kuhama makazi hayo. Katika wilaya hii iliyotangazwa "eneo la kijeshi", agizo hili lilitolewa wakati huo huo na jeshi na wanajeshi.

Mashahidi kadhaa waliripoti kukimbia kwa wakazi wa eneo la Abou Rouf ambapo nyumba kadhaa ziliathirika. Hospitali kadhaa zimekuwa zikitoa wito tangu Agosti 7 kwa ajili ya kuchangia damu mjini Khartoum, huku idadi ya hospitali zinazotoa huduma ikiendelea kupungua: asilimia 80 ya hospitali nchini humo hazina huduma, linabainisha Shirika la Afya Duniani (WHO). Zile ambazo bado zinafanya kazi mara nyingi zinalengwa na mashambulizi au uporaji, wakati mwingine wanakabiliwa na ukosefu wa kila kitu.

Idadi ya wanawake waliobakwa na watu kutekwa nyara  inaendelea kuongezeka.

Walionusurika pia wamehusisha vitendo vya utekaji nyara pamoja na ubakaji  vikosi vya FSR.

Kulingana na Souleima Ishaq al-Khalifa, daktari mkuu wa bodi ya serikali ya kupambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake, visa 108 vya unyanyasaji wa kijinsia vimerekodiwa na shirika hili huko Khartoum na Darfur. 

"Kupokea huduma muhimu za afya" baada ya ubakaji ni changamoto kubwa, anasema. Mjini Khartoum, hakuna dawa tena, na huko Nyala huko Darfur Kusini, haiwezekani wao kufika hospitali, kwa sababu kambi ya kikosi cha RSF kinawarudisha nyuma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.