Pata taarifa kuu

Senegal: Chama kikuu cha upinzani cha PASTEF cha Ousmane Sonko chavunjwa

Serikali ya Senegal imetangaza siku ya Jumatatu kufutwa kwa PASTEF, chama kikuu cha kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, chini ya saa mbili baada ya kufunguliwa mashitaka na kuwekwa kizuizini kwa kutoa "wito wa uasi na njama" dhidi ya serikali.

Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko akiwahutubia wafuasi wake wakati wa mkutano huko Ziguinchor Mei 24, 2023.
Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko akiwahutubia wafuasi wake wakati wa mkutano huko Ziguinchor Mei 24, 2023. AFP - MUHAMADOU BITTAYE
Matangazo ya kibiashara

"Chama cha kisiasa cha PASTEF kimevunjwa kwa agizo la rais", ametangaza Waziri wa Mambo ya Ndani Antoine Diome katika taarifa kwa vyombo vya habari, akihalalisha uamuzi wake kwa wito wake wa "mara kwa mara" kwa "harakati za uasi" ambazo kulingana na waziri huyo zilisababisha vifo vingi mnamo mwezi Machi 2021 na mwezi Juni. 2023. Vitisho hivi vinajumuisha “ukiukaji wa kudumu na mkubwa wa majukumu ya vyama vya siasa, " ameongeza waziri wa mambo ya ndani

Mapema siku ya Jumatatu, mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2024, alishtakiwa na jaji ambaye aliamuru azuiliwe hasa kwa "wito wa uasi na njama" dhidi ya Serikali, ameambiwa mmoja wa mawakili wake.

Siku ya Ijumaa Ousmane Sonko alikamatwa nyumbani kwake. Aliporudi kutoka kwenye swala ya Ijumaa, rais wa PASTEF alidai kuwa alimpokonya simu polisi aliyekuwa akimrekodi bila idhini yake. kitendo ambacho mamlaka nchini Senegal imekiita "wizi wa kutumia nguvu".

Hatua ya tatu ya kisheria

Ousmane Sonko, 49, kwa hivyo anaona kufunguliwa kwa utaratibu wa tatu wa kisheria dhidi yake, ambao unaweza kuhatarisha zaidi ushiriki wake katika uchaguzi wa urais wa Februari 2024.

Mwakilishi mteule wa Zinguinchor, ambaye kwa sasa yuko kwenye mgomo wa kula, tayari alihukumiwa Juni 1 hadi miaka miwili jela kwa "rushwa kwa vijana" katika kesi ambayo ilimhusisha Adji Sarr. Uamuzi wa mahakama ulisababisha ghasia na kusababisha vifo vya watu kati ya 16 na 30!

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.