Pata taarifa kuu

Niger: Makaazi ya rais Mohamed Bazoum yamezingirwa na walinda usalama

Nairobi – Makaazi ya rais wa Niger Mohamed Bazoum na afisi zake za kazi yamezingirwa na maofisa wa usalama wa kitengo maalum cha rais japokuwa taarifa ya kufanya hivyo haijaekwa wazi.

Bazoum, ambaye ni mshirika wa karibu wa Ufaransa, alichaguliwa kupitia njia ya kidemokrasia mwaka wa 2021
Bazoum, ambaye ni mshirika wa karibu wa Ufaransa, alichaguliwa kupitia njia ya kidemokrasia mwaka wa 2021 AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Niger ni mojawapo ya mataifa ya Afrika Magharibi ambayo yameonekana kutokuwa imara, ikiwa imeshuhudia mapinduzi manne ya kijeshi tangu kujipatia uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka wa 1960.

Bazoum, ambaye ni mshirika wa karibu wa Ufaransa, alichaguliwa kupitia njia ya kidemokrasia mwaka wa 2021.

Mapinduzi ya kijeshi ya mwisho kufanyika nchini humo, yalifanyika mwezi Februari mwaka wa 2010 ambapo utawala wa rais wa wakati huo Mamadou Tandja uliangushwa.

Kulifanyika jaribio jengine tarehe 31 mwezi Machi mwaka wa 2021, siku mbili tu kabla ya kuapishwa kwa rais wa sasa Mohamed Bazoum.

Watu kadhaa waliripotiwa kukamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo, akiwemo kamanda wa jeshi la angani aliyetuhumiwa kwa kupanga jaribio hilo.

Niger yenye idadi ya watu milioni 22.4 imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa makundi ya watu wenye silaha kwa muda sasa.

Makundi ya wanajihadi yanaripotiwa kutokea upande wa Mali tangu mwaka wa 2015, wakati kundi jengine likitokea kaskazini mashairki mwa Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.