Mali yakashifu hatua ya Marekani kutangaza vikwazo dhidi ya maofisa wake
Waziri mkuu wa Mali Choguel Kokalla Maïga, amekashifu hatua ya Marekani kutangaza vikwazo kwa waziri wa ulinzi nchini humo, mkuu wa jeshi la angani na naibu wake, kiongozi huyo akisistiza kuendelea kuunga mkono utawala wa kijeshi.
Imechapishwa:
Choguel amesema kuwa vikwazo dhidi ya waziri wa ulinzi Kanali Sadio Camara, Jenerali Alou Boi Diarra, Kanali Adama Bagayoko, havina malengo yoyote isipokuwa kuvuruga watu wa Mali.
Les sanctions contre nos vaillants officiers, Colonel Sadio CAMARA, Ministre de la défense, General Alou Boï DIARRA, Colonel Adama BAGAYOKO, n’ont d’autres objectifs que de divertir le peuple malien.
— Choguel Kokalla Maiga (@ChoguelKMaiga) July 25, 2023
Rien ne nous détournera du chantier de la refondation du Mali. #SOUTIEN_TOTAL pic.twitter.com/g9qFbM4tuU
Aidha kiongozi huyo ameeleza kwamba hakuna kitakachotuvuruga watu wa taifa hilo kutoka kwa malengo yake kujenga upya Mali.
Wizara ya fedha ya Marekani, ilitangaza vikwazo kwa watatu hao kwa kwa tuhuma za "kuwezesha" upanuzi wa kundi la Wagner la Urusi nchini Mali.
Wanajeshi wa Wagner wametuhumiwa kwa kufanya ukatili pamoja na jeshi la Mali katika vita vyao dhidi ya wanajihadi, huku Marekani ikisema kuwa vifo vya raia vimeongezeka zaidi ya mara tatu tangu mamluki hao walipotumwa nchini humo mwishoni mwa 2021.
Waziri mkuu ndiye afisa mkuu pekee katika serikali ya kijeshi aliyetoa maoni yake kuhusu vikwazo hivyo.