Pata taarifa kuu
CHANJO-MALARIA

Chanjo ya Malaria yaidhinishwa kwa watoto Burkina Faso

Utumiaji wa chanjo ya Malaria ya R21/Matrix-M imeidhinishwa kwa watoto wenye umri wa miezi 5 hadi 36 nchini Burkina Faso, ambako malaria ndiyo chanzo cha kwanza cha vifo vya watoto wachanga, na ambayo inakuwa nchi ya tatu barani Afrika kuiweka sokoni.

Mtoto akipokea dozi ya chanjo ya Malaria nchini Burkina Faso.
Mtoto akipokea dozi ya chanjo ya Malaria nchini Burkina Faso. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

"Chanjo ya Malaria ya R21/Matrix-M imeidhinishwa kutumika nchini Burkina Faso na shirika la kitaifa la kudhibiti dawa (ANRP) lililochini ya mamlaka ya Wizara ya Afya na Usafi wa Umma," Kitengo cha Utafiti wa Kliniki ya Nanoro (URCN), ambapo majaribio hayo yalikuwa yakifanywa, kimesema katika taarifa siku ya Jumanne.

"Kufuatia matokeo ya kwanza juu ya usalama na ufanisi wa chanjo hii iliyoripotiwa mwaka wa 2021 na timu ya URCN, tulikuwa na matumaini kuhusu idhini yake ya baadaye na tuna furaha sana kuona hii ikiidhinishwa leo", amesema Waziri wa Afya wa Burkina Fasio, Robert Kargougou, aliyenukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari. Nchini Burkina Faso, watoto wenye umri wa miezi 5 hadi 36 ndio kundi la umri lililo katika hatari zaidi ya vifo vinavyohusiana na malaria.

"Chanjo hii itakuwa chombo kipya muhimu sana ambacho kitachangia kuharakisha mpango wa kutokomeza malaria nchini Burkina Faso", amesema Bw. Kargougou, akikumbusha kwamba "malaria ni mojawapo ya sababu kuu za vifo vya watoto wachanga nchini Burkina Faso". afisa mkuu wa majaribio kwenye wizara ya Afya, Profesa Halidou Tinto, amekaribisha "uamuzi wa kihistoria ambao utasaidia kuokoa mamilioni ya maisha".

Uamuzi wa kuidhinisha chanjo hii ulitokana na matokeo ya utafiti wa awamu ya 2 na ya3 uliofanywa na URCN na ambao ulihusu baadhi ya watoto 5,000, hasa nchini Burkina Faso, majaribio mengine ambayo pia yamefanywa nchini Kenya, Mali na Tanzania.

Baada ya Ghana na Nigeria, Burkina Faso ni nchi ya tatu katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara kusajili chanjo hii inayozalishwa na kuuzwa na Serum Institute of India, SII, yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya dozi milioni 200 kwa mwaka. Mnamo mwaka 2021, Burkina Faso ilirekodi zaidi ya visa milioni 12 vya Malaria, ambapo 4,355 vilisababisha vifo, kulingana na taarifa ya magonjwa ya Wizara ya Afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.