Pata taarifa kuu

Kikosi cha maafisa wa polisi karibu na nyumba ya Ousmane Sonko chaondolewa

Maafisa wa usalama waliowekwa na mamlaka karibu na nyumba ya Dakar ya kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, mgombea wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2024, wameondolewa, mwandishi wa habari wa AFP amebainisha siku ya Jumatatu.

Kuidhinishwa kwa Ousmane Sonko kulifanyika Alhamisi wakati wa mkutano wa Mamlaka ya Juu ya Udhibiti wa chama, chombo cha PASTEF.
Kuidhinishwa kwa Ousmane Sonko kulifanyika Alhamisi wakati wa mkutano wa Mamlaka ya Juu ya Udhibiti wa chama, chombo cha PASTEF. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kikosi cha maafisa wa usalaama wameondolewa", ameliambia shirika la habari la AFP, Ousseynou Ly, msemaji wa chama cha PASTEF, ambaye alifafanua kuwa mpinzani huyo, aliyehukumiwa Juni 1 hadi miaka miwili jela kwa kesi ya maadili, alikuwa hajakamatwa. Bw. Sonko alikuwa amezuiliwa na vikosi vya usalama nyumbani kwake katika mji mkuu, "kuzuiliwa" kulingana na yeye, tangu Mei 28.

Bw. Sonko alihukumiwa Juni 1 hadi miaka miwili gerezani katika kesi ya maadili, uamuzi ambao hautamfanya awanie katika uchaguzi ujaoa, kulingana na mawakili wake na wataalamu wake wa sheria. Hukumu yake mwanzoni mwa mwezi Juni ilisababisha machafuko makubwa zaidi kwa miaka mingi nchini Senegal, ambayo yalisababisha vifo vya watu 16 kulingana na mamlaka, karibu thelathini kulingana na upinzani. Kiongozi wa Pastef kisha alitabiri katika mahojiano "machafuko yasiyoelezeka" ikiwa atazuiwa kuwa mgombea katika uchaguzi ujao wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.