Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Somalia: Zaidi ya wapiganaji mia moja wauawa katika operesheni ya pamoja na Marekani

Mamlaka ya Somalia imetangaza kuwa imewaua wanajihadi zaidi ya 100 wa Al Shabab katika operesheni ya pamoja ya kijeshi na Marekani. Kwa upande wake, Marekani inathibitisha kuwa imewaangamiza maafuisa wakuu watano wa Al-Qaeda katika operesheni hii.

Askari wa vikosi vya usalama vya Somalia, hapa wakishika doria Mogadishu, Februari 21, 2023.
Askari wa vikosi vya usalama vya Somalia, hapa wakishika doria Mogadishu, Februari 21, 2023. AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu nchini Marekani, David Thomson

Mashambulizi haya ya anga ya Marekani yalifanyika siku ya Jumatano kwa kushirikiana na wanajeshi wa Somalia katikati mwa Somalia, kulingana na AFRICOM, makao makuu ya vikosi vya Marekani barani Afrika.

Mashambulizi haya yalitekelezwa kwa ombi la mamlaka ya Somalia na kuwezesha, kulingana na Marekani, kuwaangamiza maafisa wakuu watano wa kundi la wanamgambo la Al Shabab, lenye uhusiano na al-Qaeda. Kwa upande wake, Somalia inadai kuangamiza wanajihadi zaidi ya mia moja wa kundi la Al Shabab.

Operesheni hii inakuja wiki moja baada ya shambulio lingine la Marekani lililoua wanajihadi 10 katika eneo la Afmadow kusini mwa nchi hiyo.

Mashambulizi ya Marekani dhidi ya wanajihadi wa Somalia hufanyika mara kwa mara. Mwezi Mei mwaka jana, Rais Joe Biden aliidhinisha ombi la Pentagon la kupeleka wanajeshi 500 wa Marekani kupambana na makundi ya kigaidi yanayoendesha uhalifu nchini Somalia. Kutumwa kwa jeshi la Marekani kulilochochewa wakati huo na hofu ya Ikulu ya White House kuona Al Shabab wakiwashambulia raia wa Marekani na maslahi ya Marekani katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.