Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Burkina Faso: Vijana wamiminika mitaani baada ya 'kutekwa nyara' kwa mbunge wa zamani

Nchini Burkina Faso, mamia ya vijana walifanya maandamano usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, katika viunga vya kusini mwa mji mkuu. 

Mwanajeshi wa Burkinabe akipiga doria katika mji wa Ouahigouya, mkoa wa Yatenga, Oktoba 29, 2018.
Mwanajeshi wa Burkinabe akipiga doria katika mji wa Ouahigouya, mkoa wa Yatenga, Oktoba 29, 2018. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Waliweka vizuizi usiku kucha kuzuia shughuli ya uchukuzi kwenye Barabara ya kitaifa nambari 6 kupinga kile wanachokichukulia kuwa utekaji nyara wa aliyekuwa mbunge, na meya wa mji wa Komsilga, ulioko takriban kilomita ishirini kutoka mji mkuu. 

Kulingana na Muungano wa Maendeleo na Mabadiliko, chama ambacho aliyekuwa mbunge na meya wake, Issouf Nikiema alitekwa nyara na watu waliovalia wlio jifunika nyuso katikati ya mji wa Ouagadougou, alipokuwa akienda kuswali swala ya Ijumaa. Chama hicho kinaomba mamlakaitoe mwanaga kuhusiana na jambo hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.