Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

DRC: Wagombea kwenye nafasi za ubunge wana siku saba za kuwasilisha faili zao

Nchini DRC, Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) imeongeza kwa wiki moja makataa ya kuwasilisha wagombea kwenye nafasi ya ubunge wa kitaifa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Desemba 20, 2023. Ofisi za uandikishaji zilizofunguliwa tangu Juni 25, zilipaswa kufungwa Jumamosi Julai 15. Hatimaye, zitaendelea kuwa wazi hadi Jumapili Julai 23, 2023. Haya yamefikiwa katika mkutano wa Jumamosi Julai 15 ambapo CENI ilitangaza uamuzi wake.

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha faili kwa wagombea kwenye nafasi ya ubunge nchini DRC imeosogezwa mbele hadi tarehe 23 Julai 2023.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha faili kwa wagombea kwenye nafasi ya ubunge nchini DRC imeosogezwa mbele hadi tarehe 23 Julai 2023. JUNIOR D.KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, katika siku za hivi majuzi, Mwenyekiti wa CENI, Denis Kadima, alionya wazi kwamba hakutakuwa na muda wa ziada. Hatimaye, siku saba zaidi zimetolewa kwa wagombea ambao hawajakamilisha faili zao.

CENI yenyewe ilitambua hili katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ikirejelea baadhi ya afisi ambazo hazijasajili mgombea hata mmoja na zinine zimesajili wagombea wachache. Katika mkoa wa Tshopo, kwa mfano, wiki hii, gavana aliwataka wagombea hao kuharakisha, huku akibainisha wakati wa ziara yake katika ofisi ya CENI kuwa ni faili tatu tu ndizo zimewasilishwa, kwazaidi ya viti kumi.

Kwa upande wa baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wanasema, kulikuwa na ukosefu wa maandalizi kwa upande wa vyama, na wakati mwingine makataa mafupi ya kukusanya nyaraka zote muhimu kwa faili.

Na kisha, baadhi ya vyama vikuu vilijiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi. Hii ni kesi ya vyama kadhaa vya kisiasa vinavyounda muungano wa FCC, wa rais wa zamani Joseph Kabila, lakini pia kwa Ecide, chama cha Martin Fayulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.