Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

DRC: Polisi yamhoji dereva wa Chérubin Okende siku moja baada ya mauaji yake

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), baada ya kifo cha mbunge wa upinzani Chérubin Okende, uchunguzi umefunguliwa. Mshukiwa aliyekamatwa Alhamisi, Julai 13 si mwingine, bali ni afisa wa polisi na mlinzi aliyeandamana na mbunge huyo Jumatano alasiri katika Mahakama ya Katiba, ambako alikuwa akienda kuomba kuahirishwa kwa kusikilizwa kwake kuhusu kauli yake ya mirathi kama waziri wa zamani. Ijumaa, Julai 14, mtu wa pili alifikishwa mikononi mwa polisi kama sehemu ya uchunguzi.

Mbunge na waziri wa zamani Chérubin Okende, Februari 25, 2023, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa.
Mbunge na waziri wa zamani Chérubin Okende, Februari 25, 2023, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa. © Pascal Mulegwa / RFI
Matangazo ya kibiashara

Wakati huu, dereva wa Chérubin Okende yuko chini ya kifungo cha nyumbani, anaripoti mwandishi wetu mjini Kinshasa, Pascal Mulegwa.

Kufikia sasa, mlinzi huyo ndiye pekee aliyethibitisha kuwa mbunge huyo alikuwa ameegeshwa gari mbele ya Mahakaam ya Katiba, na mahakama imetoa wito kwa mashahidi kuja kushuhudia yale waliyo yaona wakati wa tukio hilo.

Kwa sasa, uchunguzi wa kimahakama unachunguzwa na Mahakama Kuu ya Kinshasa-Gombe, ingawa uhalifu huo ulifanywa kwa kutumia silaha. Serikali imeamua kuhusisha vyombo vyote vya usalama na wachunguzi wanajaribu kuangazia mazingira ya kutoweka kwake saa kadhaa kabla ya kupatikana kwa mwili wake. Wito pia umezinduliwa kujaribu kutafuta mashahidi walio kuwepo katika eneo la Mahakama ya Kikatiba siku ya Jumatano.

Wachunguzi kutoka Ubelgiji na Afrika Kusini waitwa kusaidia

Ikiombwa mara kwa mara na mamlaka za mahakama, Ofisi ya Pamoja ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (BCNDUH) bado haijapokea ombi la uchunguzi wake, hasa katika utaratibu wa kimahakama. BCNDUH ilmesema imekuwa ikifuatilia faili hiyo "kwa karibu sana" tangu kutoweka kwa Chérubin Okende.

Mamlaka ya Kongo imeomba msaada kutoka kwa mataifa ya kigeni. Wachunguzi wanapaswa pia kupata msaada kutoka nchi "rafiki", kama alivyosema msemaji wa serikali Patrick Muyaya siku ya Alhamis.

Chanzo kinachofahamu suala hilo sasa kinataja ushiriki wa wachunguzi wa Ubelgiji na Afrika Kusini. Taarifa hizo zilithibitishwa na chanzo cha kidiplomasia cha Ubelgiji ambacho kinaongeza kuwa Waziri Mkuu Alexander De Croo ametangaza nia yake ya kuunga mkono DRC katika uchunguzi huo, akisubiri taarifa zaidi kuhusu masharti ya usaidizi huu.

Maaskofu wa Kongo watoa wito kwa vyama vya kisiasa 'kuwajibika'

Miongoni mwa athari zilizochochewa na uhalifu huu, Baraza la Maaskofu wa Kongo (Cenco) linasema limesikitishwa na mauaji yasiyoelezeka. Pia limeelezea kuchukizwa na hali mazingira mabaya ya kisiasa na linatoa wito kwa uwajibikaji wa vyama vya siasa, hasa "katika muktadha huu wa maandalizi ya uchaguzi".

Mashirika ya kiraia yanataka uchunguzi wa kuaminika na wa kina. Chama cha Kijamii cha New Kongo (NSCC) kinaomba kuhusishwa na tume hii ya uchunguzi ili kutofanya makosa kama siku za nyuma: Jonas Tshiomela, mratibu wa NSCC, anakumbusha kesi ya Floribert Chebeya, mwanaharakati wa haki za binadamu na mwanzilishi wa Voix des sans voix (Saiti ya Wanyonge) aliyeuawa mnamo mwezi Juni 2010 katika mazingira kama haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.