Pata taarifa kuu

Jacob Zuma yuko nchini Urusi kwa ajili ya kupokea matibabu

Wakfu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, umesema kiongozi huyo yuko jijini Moscow nchini Urusi kwa sababu za kimatibabu.

Mahakama ya kikatiba nchini Afrika Kusini inataka kiongozi huyo kurejea gerezani
Mahakama ya kikatiba nchini Afrika Kusini inataka kiongozi huyo kurejea gerezani AFP - EMMANUEL CROSET
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wakfu huo, Zuma atarejea nchini mwake wakati ambapo madaktari wake watakuwa wamemaliza kumhudumia.

Haya yanajiri siku moja baada ya kiongozi huyo wa zamani nchini humo kupoteza ombi lake katika mahakama ya kikatiba kubatilisha agizo la kurejeshwa gerezani.

Rais huyo wa zamani alisafiri kwenda Urusi kwa kutumia ndege ya umma wiki iliyopita kwa mujibu wa msemaji wa wakfu huo Mzwanele Manyi.

Mahakama ya kikatiba alhamis ya wiki hii katika uamuzi wake ilisema kwamba Zuma aliruhusiwa kuondoka gerezani kwa ajili ya kupokea matibabu kinyume na sheria.

Zuma aliachiwa huru mwezi Septemba mwaka wa 2021 baada yake kukaa gerezani kwa wiki nane kati ya kifungo cha miezi 15 alichokuwa amepewa.

Alikuwa amepatikana na hatia baada yake kukataa kushirikiana na uchunguzi dhidi ya ufisadi katika kipindi chake cha uongozi.

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) kimekaribisha uamuzi wa mahakama hiyo, kikisema kwamba kinathibitisha kuwa Zuma "anafaa kuwa gerezani".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.