Pata taarifa kuu

Hatua zinahitajika kumaliza ufisadi katika nchi za Afrika ya kati na magharibi: Amnesty

Nairobi – Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International katika taarifa yake limesema kwamba mataifa ya Afrika Magharibi na ya kati zinahitaji kufanya juhudi zaidi kupiga vita rushwa pamoja na kuwasaliti wateteza wa haki za binadamu wanaofichua uhalifu huo na kuupinga.

Amnesty International
Amnesty International @សហការី
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake ya siku ya kupambana na ufisadi barani Afrika, shirika hilo limekashifu matukio ya kukamatwa, kunyanyaswa, kuzuiliwa, kupigwa faini za juu na hata wakati mwengine kuawaua kwa watetezi wa haki za binadamu wanaopiga vita rushwa katika mataifa 19 ya Afrika Magharibi na ya kati.

Amnesty International imetolea mfano mwanahabari wa Cameroon Martinez Zogo, ambaye kwa mujibu wa shirika hilo alikuwa anachunguza ubadhirifu wa mamia ya mabilioni ya pesa za taifa hilo na watu wa karibu na maofisa wa serikali.

Zogo alitekewa na watu wasiojulikana tarehe saba ya mwezi Januari kabla ya mwili wake kupatikana nje ya jiji kuu.

Nchini Togo, mwanahabari mwengine kwa jina la  Ferdinand Ayite alikamatwa tarehe 10 ya mwezi Desemba mwaka wa 2021 baada yake kuwahusisha maofisa wawili wa serikali na ufisadi.

Ayite alihukumiwa jela tarehe 15 ya mwezi Machi pamoja na wafanyikazi wenzake miaka mitatu na faini ya pesa za taifa hilo milioni tatu kwa tuhuma za kueneza habari za uongo dhidi ya mamlaka, imesema taarifa ya Amnesty.

Licha ya Ayite na wenzake kukata rufa dhidi ya uamuzi huo, walilazimika baadae kutoroka nchini humo wakihofia usalama wao.

Mataifa hayo yametakiwa kuweka sheria kali zinazopinga vitendo vya utoaji wa rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.