Pata taarifa kuu

WAEMU yafuta hatua ya Mali kusimaishwa kwenye taasisi zake

Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (UEMOA) umetangaza kufuta hatua ya kusimamishwa kwa Mali kwenye taasisi zake, iliyochukuliwa mwezi Januari 2022, ili kuadhibu nia ya utawala wa kijeshi kusalia madarakani kwa miaka kadhaa zaidi.

Mkutano usio kuwa wa kawaida wa WAEMU ulifanyika mjini Bissau mnamo Julai 8, 2023.
Mkutano usio kuwa wa kawaida wa WAEMU ulifanyika mjini Bissau mnamo Julai 8, 2023. © RFI/Serge Daniel
Matangazo ya kibiashara

WAEMU imechukua uamuzi huu wakati wa kikao kisicho cha kawaida kilichofanyika Jumamosi nchini Guinea-Bissau, ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyopokelewa na shirika la habari la AFP siku ya Jumapili.

"Kuhusu Mali, Mkutano uliamua kufuta hatua ya kusimamishwa kwake kwenye taasisi za WAEMU, hatu iliyochukuliwa mnamo Januari 9, 2022", WAEMU imetaangaza, bila maelezo zaidi.

Mwezi Januari 2022, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na WAEMU waliweka hatua kali za kiuchumi na kidiplomasia dhidi ya Mali ili kuadhibu nia ya serikali ya kijeshi kuendelea kuwa madarakani kwa miaka mitano.

ECOWAS iliondoa vikwazo vya kibiashara na kifedha mnamo mwezi Julai 2022, ikithibitisha ratiba mpya iliyopendekezwa na serikali kuu ya kipindi cha mpito kinachodumu hadi Machi 2024.

Mali pia ilisimamishwa kutoka kwa vyombo vya maamuzi vya ECOWAS baada ya kuchukua mamlaka mnamo 2020.

Kiongozi wa kijeshi wa Mali Assimi Goita alichukua mamlaka mnamo mwezi Agosti 2020 na kisha kuunda serikali ya mpito inayoongozwa na raia.

Mnamo mwezi Mei 2021, aliwaondoa viongozi hao wa kiraia katika mapinduzi ya pili, na baadaye kuapishwa kama kaimu ya rais wa Mali.

Mnamo mwezi Juni, wananchi wa Mali waliidhinisha kwa wingi rasimu ya Katiba mpya, hatua muhimu katika kufikia kilele Machi 2024 kwa kurudi kwa raia kwa mkuu wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.