Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Burkina: Watu 16 wanaojitolea kwa ulinzi wa taifa na raia 2 wauawa katika shambulio

Nchini Burkina Faso, Wanamgambo wasiopungua 20 wa kujitolea kwa ajili ya ulinzi wa nchi (VDP) na raia wawili waliuawa siku ya Ijumaa Julai 7 wakati wa shambulio katika eneo linlopatikana kilomita thelathini mashariki mwa Boulsa. Kijiji cha Kogsablego ndicho kililengwa na shambulio hili jipya. 

Mnamo Oktoba 8, wanajeshi wa Burkina Faso walizika wenzao waliokufa wakati wa shambulio huko Gaskinde.
Mnamo Oktoba 8, wanajeshi wa Burkina Faso walizika wenzao waliokufa wakati wa shambulio huko Gaskinde. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji pia walichoma moto soko na maduka. Wahanga walizikwa Jumamosi hii katika wilaya ya Boulsa katika mkoa wa Center-North. Washambuliaji kumi na wawili waliangamizwa na VDP, wasaidizi wa kiraia wa vikosi vya jeshi.

Burkina Faso, mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani, inapambana na uasi wa wapiganaji wa kiislamu ambao ulianzia nchini Mali mnamo mwaka wa 2015, na imeshuhudia zaidi ya raia 10,000, wanajeshi na polisi wakiuawa, kulingana na takwimu za shirika moja lisilo la serikali,

Takriban watu milioni 2 wamelazimika kuyahama makazi yao.

Hasira ndani ya jeshi kwa kushindwa kudhibiti uasi huo, zilisababisha mapinduzi mawili nchini Burkina Faso mwaka jana.

Mashambulizi manne ya watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi nchini Burkina Faso yaliwauwa wanamgambo 40 wa kujitolea, na wanajeshi 39 wa kawaida wiki iliyopita, jeshi na vyanzo vya usalama vilisema.

Mapigano mawili mabaya zaidi yalitokea katika eneo la Center-North mnamo tarehe 26 mwezi Juni na taarifa za awali zilielezea kwamba dazani za watu waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.