Pata taarifa kuu

Mali: Wanasiasa wapokea kwa hisia tofauti uamuzi wa kuondolewa kwa MINUSMA

MINUSMA itaondoka Mali mwishoni mwa mwaka huu, kwa hivyo ina miezi sita ya kufungasha virago. Mali ililitaka wiki mbili zilizopita kuondoka kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio siku ya Ijumaa kuthibitisha uamuzi huu. Uamuzi uliokaribishwa kwa hisia tofauti na wanasiasa nchini Mali.

Ujumbe wa MINUSMA kaskazini mwa Mali. "Kaskazini, eneo ambalo ililindwa na wanajshi wa MINUSMA na jeshi la Mali, litakuta liko peke yake, itakabidhiwa kwa magaidi", anasema mpinzani Ismaël Sacko.
Ujumbe wa MINUSMA kaskazini mwa Mali. "Kaskazini, eneo ambalo ililindwa na wanajshi wa MINUSMA na jeshi la Mali, litakuta liko peke yake, itakabidhiwa kwa magaidi", anasema mpinzani Ismaël Sacko. MINUSMA/Marco Dormino
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya siasa na mashirika yanayo unga mkono mamlaka ya mpito ya Mali wanafurahi, machoni pao ni kitendo kipya cha nguvu cha uhuru. Miongoni mwao ni Mohamed Bill Traoré, kiongozi wa chama cha Ensemble Sauvons le Mali na msemaji wa vuguvugu la Yerewolo-Debout, anayeunga mkono kwa dhati wanajeshi walioko madarakani mjini Bamako na ambaye kwa muda mrefu alitaka kuondoka kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali: “ Furaha ilioje kwetu, kwa raia wa Mali na pia kwa raia wa Afrika," amesema, akielezea kusikitishwa kwake na hasira yake kuona miaka kumi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa inamalizika bila kuwepo na usalama tosha nchini Mali: "Tulifikiri kwamba MINUSMA walikuja kusaidia mamlaka ya Mali. Lakini ilishindwa kuilinda nchi, na ikajitolea misheni nyingine! Mbaya zaidi ni ripoti zake za uongo na kashfa dhidi ya mamlaka ya Mali. "

Akirejelea ripoti za Umoja wa Mataifa ambazo zinalishutumu jeshi la Mali na wasaidizi wake wa Urusi kwa unyanyasaji dhidi ya raia wa Mali, madai ambayo Bamako inafutilia mbali: "Madhumuni ya ripoti hizi, anasema msemaji wa vuguvugu la Yerewolo, ni kuitia hatiani mamlaka ya Mali, ambayo jukumu lake kubwa ni kutetea matarajio ya kweli ya raia wa Mali. Shirika lolote linalojaribu kushutumu mamlaka ya Mali, watu hawawezi kukaa kimya waliksikilza  au kulitazama! "

Wasiwasi kwa upande wa upinzani

Shauku ya kuungwa mkono na mamlaka ya Mali ya mpito, wasiwasi na machafuko kwa upande wa upinzani. Ismaël Sacko ni rais wa PSDA, chama ambacho mahakaam ya Mali iliamuru kufutwa mnamo Juni 14, ndani ya mfumo wa utaratibu ulioanzishwa na serikali ya Mali; PSDA ilikata rufaa uamuzi huu. "Katika ngazi ya kidiplomasia, anaelezea, Mali itajikuta imetengwa zaidi," amesema mpinzani aliye uhamishoni nje ya Mali, "kwa sababu mamlaka ya mpito, wanajeshi waliomalakani nchini Mali, inapaswa kuchukua fursa ya uwepo wa MINUSMA kuimarisha uhusiano wake pamoja na nchi zinazochangia mijadala mbalimbali, lakini ni kinyume kabisa (kilichotokea, maelezo ya mhariri). Sio Wagner pia ambaye atailinda Mali: haina njia zote muhimu, haidhibiti ardhi yoyote, na Wagner, kwa bahati mbaya sana, inaonekana leo na raia wa Mali kama nguvu hatari. inaua watu wetu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.