Pata taarifa kuu

Mali: Asilimia 97 ya wapiga kura waliunga mkono rasimu ya katiba mpya

Nairobi – Nchini Mali, raia walipiga kura kuidhinisha rasimu ya katiba mpya katika zoezi lililofanyika tarehe 18 ya mwezi Juni ambapo asilimia 97 ya wapiga kura waliunga mkono mchakato huo kwa mujibu wa tume ya uchaguzi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Raia wa Mali walipiga kura kuidhinisha rasimu ya katiba mpya
Raia wa Mali walipiga kura kuidhinisha rasimu ya katiba mpya © Colonel Assimi GOITA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa utawala wa kijeshi nchini humo, hatua hiyo sasa inatoa nafasi ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi Februari mwaka ujao, hatua itayorejesha nchi hiyo katika utawala wa kiraia.

Mkuu wa tume ya uchaguzi Moustapha Cisse amesema chini ya asilimia 40 ya wapiga kura kati ya 8.4 ndio waliojotekeza kushiriki zoezi hilo.

Mali imeshuhudia mapinduzi mawili ya kijeshi tangu mwezi agosti mwaka wa 2020 wakati utawala wa  rais Ibrahim Boubacar ulipoangushwa.

Serikali ya kijeshi inasema hatua hiyo inalenga kurejesha utawala wa kiraia
Serikali ya kijeshi inasema hatua hiyo inalenga kurejesha utawala wa kiraia © OUSMANE MAKAVELI / AFP

Kiongozi wa kijeshi ambaye pia ni rais wa mpito Assimi Goïta alisema katika hotuba yake kwamba "anashawishika kwamba kura hii ya maoni inafungua njia kwa Mali mpya, yenye nguvu, yenye ufanisi na inayoibukia, lakini zaidi ya yote Mali katika huduma ya ustawi wa watu".

Kabla ya kura hiyo ya maoni kulikuwa na wasiwasi kwamba katiba mpya ingempa mamlaka makubwa rais ambaye sasa atakuwa na haki ya kuajiri na kumfukuza kazi waziri mkuu na wajumbe wa baraza la mawaziri.

Mabadiliko hayo ya katiba pia yanaitaja Mali kama taifa lisilo na dini, hatua iliyopingwa na baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.